Wednesday, July 02, 2014

SAFARI YA MCHUJO KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) YAANZA RASMI

 Jukwaa likitengenezwa kwaajili ya Washiriki Wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kupanda jukwaani na kuanza kuonyesha vipaji vyao, Onyesho hili ni onyesho la kwanza la kuelekea Kwenye Mchujo wa kumpata mshiriki Mmoja atakayejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza
Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa usiku huu
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.Picha zote na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza – Proin Promotions – Dar Es Salaam.
Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza.  Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.

Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno “TMT” kwenda namba 15678

Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno “TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki” kwenda namba 15678

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...