Thursday, July 31, 2014

SKYLIGHT BAND YAFUNIKA MBAYA EID MOSI NDANI YA ESCAPE ONE!

DSC_0011
Sam Mapenzi (katikati) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya fukwe za Escape One katika show maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid-El Fitr huku akipewa back Vocal na Sony Masamba pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0015
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Escape One.
DSC_0306
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakiachia kwenye dancing floor.
DSC_0243
Sam Mapenzi akitoa burudani adimu mashabiki wa Skylight Band katika sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One jijini Dar.
DSC_0237
Skylight Band ni #balsaa# hebu angalia mashabiki wanaojua burudani ya muziki wa Live wanavyosebeneka.
DSC_0189
Rappa Mkongwe Joniko Flower akitunzwa wekundu wa msimbazi na mmoja wa mashabiki wa Skylight Band aliyekunwa na uimbaji wa rapa huyo.
DSC_0018
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni Mary Lucos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
DSC_0466
Mary Lucos wa Skylight Band akiwaduarisha mashabiki wa bendi hiyo katika sikukuu ya Eid El Fitr ndani kiota cha Escape One.
DSC_0487
Wadada wakijipinda kuzungusha nyonga zao.
DSC_0471
DSC_0139
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiduarika.
DSC_0159
DSC_0023
Pichani juu na chini ni sehemu ya umati wa wakazi wa Dar wake kwa waume waliokusanyika ndani ya fukwe za Escape One kujipatia upepo mwanana huku wakiburudishwa na Skylight Band.
DSC_0024
DSC_0028
Mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali huku wakisiliza burudani ya kutoka bendi ambayo kwa sasa ndio habari ya mujini.
DSC_0077
DSC_0337
Ale Mama mupe Saluti……!!! Twende kazi…..
DSC_0355
Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma….Yachuma chuma…!! Kikosi cha Skylight Band wakicheza sambamba na mashabiki wao katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One.
DSC_0356
DSC_0388
Burudani ikiendelea na watu wakiendelea kusebeneka.
DSC_0401
Wadada walichizikaje…!?
DSC_0514
DSC_0411
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakionyesha umahiri wao wa kucheza moja ya staili za bendi hiyo kwa wanamuziki Joniko Flower na Sony Masamba.
DSC_0420
DSC_0235
Daudi Tumba akitweta jasho kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki kupitia ala za Band hiyo huku Tumba ikihusika pia kutengeneza sauti nzuri kabisa.
DSC_0274
Pichani juu na chini ni Hashim Donode a.k.a Mzee wa Viduku akifanya yake!
DSC_0310
DSC_0069
Afisa Mtendaji Mkuu wa Skylight Band, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi hiyo Justine Ndege wakati Skylight Band ikiendelea kutoa burudani kwenye sherehe za sikukuu ya Eid -El- Fitr ndani ya kiota cha Escape One.
DSC_0217
Blogger William Malecela a.k.a LEMUTUZ mwandaaji wa Instagram Party itakayofanyika Jumamosi hii kwenye kiota cha Escape One akishow love na Fans wake mdau Joseph Magige.
DSC_0437
Sam Mapenzi kwenye ukodak na Customer care huku akionyesha Video mpya ya “Pasua Twende” kupitia simu yake ya kiganjani.
DSC_0394
Emma Bass wa Skylight Band (kulia) akipata ukodak na swahiba wake.
DSC_0379
Joniko Flower wa Skylight Band akishow love na mdau.
DSC_0296
Mratibu wa Skylight Band Lubea akipata ukodak na Mwimbaji Mary Lucos back stage.
DSC_0002
Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band na Rais wa #WANAMANYOYA# Justine Ndege (katikati) akipata Ukodak Mkuu wa Itifaki wa #WANAMANYOYA# Eddie Viede pamoja na mdau wa Skylight Band James Rock Mwakibinga.
DSC_0228
Palinogaje wewe tu umekosekana….Si haba kesho pia ni siku tukutane viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0256
DSC_0251
Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Komando Kipensi akishow love na Tophy mpiga bass wa Skylight Band back stage.

Picha Maalum Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Asali Swala ya Iddi El Fitr katika Msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam  juzi asubuhi.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam juzi asubuhi. Picha na Freddy Maro-IKULU

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...