Thursday, October 31, 2013

BADO BODABODA 370 NA TSH MILIONI 298 KUSHINDANIWA "TIMKA NA BODABODA"‏

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Bw. Matina Nkurlu (kushoto) akiwasiliana na mmoja wa washindi kati ya (60) waliojishindia Bodaboda na (24) wamejishindia fedha taslimu katika Promosheni ya “Timka na Bodaboda” ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544. Katikati ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid na kulia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bakari Abdallah.



Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Bw.…



Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Bw. Matina Nkurlu (kushoto) akiwasiliana na mmoja wa washindi kati ya (60) waliojishindia Bodaboda na (24) wamejishindia fedha taslimu katika Promosheni ya “Timka na Bodaboda” ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544. Katikati ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid na kulia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bakari Abdallah.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Bw. Matina Nkurlu (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya Promosheni ya "Timka na Bodaboda" . Jumla ya washindi (60) wamejishindia Bodaboda na (24) wamejinyakulia fedha taslimu katika Promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544. Katikati ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid na kulia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bakari Abdallah.
Mshindi wa Promosheni ya "Timka na Bodaboda" Bw. Ernest Thawe, ambaye ni mfanyakazi wa Msimbazi Center kitengo cha ufundi wa bomba, akihesabu kitita chake cha shilingi 1,000,000 mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA na kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kushoto) katikati ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid. Jumla ya washindi (60) wameshinda Bodaboda na (24) wamejinyakulia fedha taslimu katika Promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Mshindi wa Promosheni ya "Timka na Bodaboda" Bw. Ernest Thawe, ambaye ni mfanyakazi wa Msimbazi Center kitengo cha ufundi wa bomba (kulia) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, wakiwaonesha ujumbe wa M-PESA wa shilingi 1,000,000 kwa waandishi wa habari aliotumiwa baada ya kujishindia kupitia promosheni hiyo toka makao makuu ya Vodacom. Jumla ya washindi (60) wameshinda Bodaboda na (24) wamejinyakulia fedha taslimu katika Promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Mkazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam Paul Muro ambaye ni  mmoja kati ya washindi (24) waliojishindia fedha taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000 kila mmoja katika Promosheni ya "Timka na Bodaboda" inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akihesabu kitita chake huku akiwa na bashasha baada ya kujishindia kiasi hicho huku akishuhudiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Matina Nkurlu.

VIONGOZI MBALIMBALI WA KISERIKALI WAMZIKA MAREHEMU BALOZI SEPETU HAPO JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
 Shein akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar
 Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi
 Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi
 Unguja jana.…

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed 
Shein akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar
 Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Baloz
i Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi
 Unguja jana.
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na 
Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini 
kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
Padri wa Kanisa Katoliki la  Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani 
Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,
wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi 
Unguja jana.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,ukitemshwa katika
 kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya 
 Magharibi Unguja jana.
( PICHA RAMADHAN OTHMAN IKULU )

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI NSSF WATEMBELEA MIRADI YAO‏


Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakitembelea mradi wa nyumba za bei nafuu eneo la Mtoni Kijichi.

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kulia waliokaa mezani) akitoa taarifa fupi kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi Karim Mattaka (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na maofisa wa NSSF wakiteremka kwenye gari katika moja ya miradi ya taasisi hiyo walipotembelea jana.

Mmoja wa maofisa wa juu na mhandisi kutoka NSSF akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi.

Mfisa Mradi msimamizi na Msanifu wa NSSF, Deogratias Mponeja (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya mradi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba nafuu kwa wajumbe.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kulia) akiwa na Eunice Chiume wakizungumza jambo katika ziara ya wajumbea wa Bodi ya NSSF kutembelea miradi jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa Mradi na Msanifu Majengo wa NSSF, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub (aliyesimama) akitoa taarifa fupi juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa wajumbw wa bodi.

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu uliopo eneo la Mtoni Kijichi na ujenzi wa Daraja la Kisasa eneo la Kigamboni.

Akitoa taarifa fupi kwa wajumbe wa bodi ya NSSF wakiwa eneo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu na za kisasa eneo la Mtoni Kijichi, Mkurugenzi wa Mipango, Miradi na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub Kidula alisema eneo hilo linatekelezwa kwa awamu mbili za ujenzi wa nyumba aina mbalimbali.

Alisema awamu ya pili ambayo iliendelea baada ya kukamilika ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 85, imetekelezwa kwa ujenzi wa nyumba 215 eneo la Mtoni Kijichi mradi ambao tayari umekamilika na nyumba zimeanza kuuzwa kwa wanachama wa NSSF. Alisema nyumba 200 tayari zimekamilika huku 15 zilizosalia zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Alisema tayari Shirika hilo limeanza kutekeleza ujenzi mwingine wa awamu ya tatu utakaowezesha ujenzi wa nyumba za kisasa na bora zaidi zenye uwezo wa kuchukua familia 820 zikiwa na ghorofa moja huku zikiwa zimeboreshwa zaidi kihuduma ukilinganisha na zilizojengwa awali.

Aidha akifafanua juu ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zinazoendelea kujengwa na NSSF, alisema mbali na kuwa za bei ya chini zinahuduma muhimu za kijamii kama umeme, maji, mfumo mzuri wa kuifadhi maji taka, eneo la nje la ziada pamoja na vifaa vingine zikiwemo feni vyumba vyote, mfumo wa maji ya moto kwenye mabafu na sakafu ya kisasa 'tiles'.

Alisema nyumba zinazojengwa zinaukubwa na idadi ya vyumba tofauti kulingana na maitaji ya mteja, yaani kuanzia vyumba viwili hadi vitatu vya kulala huku vyote vikiwa na sebule, jiko, choo pamoja na stoo. Aliongeza kuwa milango na madirisha yamejengwa kwa vioo na chuma (nondo) ili kuimarisha zaidi kiusalama huku jiko likiwa na kabati maalumu na za kisasa kwa ajili ya kuifadhia vitu.

Kidula alisema nyumba ya chini itauzwa takribani sh milioni 66 za kitanzania bei hiyo ikiwa ni pamoja na VAT. Wajumbe wa bodi pia walitembelea mradi mkubwa wa NSSF wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambao unafanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Serikali.

Akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Meneja Mradi huo, Mhandisi Karim Mattaka alisema licha ya ujenzi huo kuendelea vizuri kwa sasa zipo changamoto kadhaa za ujenzi ambazo zilijitokeza hivyo kushughulikiwa mara moja.

Alisema daraja hilo la kisasa litakalokuwa na njia (barabara sita) yaani tatu za kwenda Kigamboni na tatu za kurudi linatarajiwa kuunganishwa kisasa na barabara ya Mandela huku likiwa na njia za kutosha kuzuia msongamano wa magari. Akizungumzia ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi, Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume alisema ni ziara ya kawaida ya wajumbe hao kukagua miradi ya taasisi hiyo na huenda ziara hiyo ikawa na manufaa ya punguzo la riba kwa wanachama wanunuzi wa nyumba hizo.

Saini zakusanywa kumng’oa Makinda

makinda+px-2Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk. Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda.Kusoma zaidi Read more »

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA POLISI KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NA UFUNDI....TAZAMA MAJINA HAPA



Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu walioorodheshwa hapa chini wa vyuo vya Elimu ya Juu na  vya Ufundi  Stadi. 
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni kila siku kwa taaluma na maeneo yafuatayo;
  •  Fani za Menejimenti  ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. Usaili  wa fani hizi  utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
  • Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa  fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani  TEHAMA KEKO chini.
  • Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
  • Waataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Orodha  ya majina inapatikana  pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe  04/11/2013.
   Muhimu: 
  1. (i)Mwombaji afike kwenyeakiwa na nakala  halisi  pamoja na kivuli cha  vyeti vyote vya masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani  kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa.Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 
  1. (ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharamaupimaji afya  shilingi elfu kumi(10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili.
 (iii)Kwa kuwa  muda ni mchache  anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa  atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.
 Orodha ni kama ifuatavyo;

BOFYA HAPO CHINI UDOWNLOAD MAJINA
-http://www.policeforce.go.tz

Mahakama ya Rufaa yasikiliza maombi ya ‘Babu Seya’ na ‘Papii Kocha’


 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza ‘Papii’ wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia hukumu iliyoitoa mwaka 2010.
 Nyuso za matumaini…….
bofya
 Johnson  Nguza ‘Papii’ akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.
 Papii akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
 Waandishi wa habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani hapo.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakati wakitoka mahakamani.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Watu waliohudhuria mahakama hapo wakifuatilia kesi hiyo.
 Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.  
 Mahakamani.
Nguza Vicking ‘Babu Seya’ akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.

Picture
Nguza Vicking na mwanaye Johnson Nguza katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa ya kesi yao. (Picha: Francis Dande)
Na HAPPINESS KATABAZI, Tanzania Daima

MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Johnson Nguza 'Papi Kocha Mtoto wa Mfalme', wameiomba Mahakama ya Rufaa nchini iifanyie upya hukumu yake iliyoitoa Februali mwaka 2010 ambayo iliwahukumu kifungo cha maisha kwasababu hukumu hiyo ina utetelezi wa wazi wa kisheria.

Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba yao na wakili wao Mabere Marando jana mbele ya jopo lilelile lilotoa hukumu ya awali ya Februali 2010  ambalo linaongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk .S.Mbarouk.

Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009  inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa  hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini  mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake.

Wakili Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 ,   ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi, litaja  moja ya utelezi wa wazi wazi wa kisheria uliofanywa na mahakama hiyo, ni kwamba katika hukumu hiyo  kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosoea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto waliokuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo na kwamba mahakama ya rufaa ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono ndiyo walioutumia kuwatia hatiani waomba rufaa kwa adhabu ya kifungo cha maisha.

“Waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi  kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii;

“Nafahamu ni kazi ngumu sana  kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu’ alidai Marando.

Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo,Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010.

Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari.

“Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”alidai wakili  Jackson.

Aidha Jaji Kimaro alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili akaamuru waomba rufaa warejeshwe gerezani na kwamba mahakama itatoa tarehe ya kutoa uamuzi wake kuhusu maombi hayo kwa pande zote mbili.

Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Addy Lyamuya, aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na jopo hilo la majaji wa tatu linaloundwa na Jaji Kimaro ,Massati na Mbarouk liliwatia hatiani kwa makosa ya kuwabaka watoto wadogo na likawahukumu kifungo cha maisha gerezani na hadi sasa wameishakaa gerezani kwa miaka kumi.

Mahakama ya Rufaa, Februali mwaka 2010 ,ilirekebisha hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu ambapo iliwaachiria huru waomba rufaa wawili katika kesi hiyo  ambao ni watoto wa Nguza Vicking, Nguza Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru, huku Viking na Papi Kocha wakiendelea kutumikia kifungo chao hadi sasa.

Hata hivyo jana mahakama hiyo ilifurika wanamuziki, mashabiki, ndugu wa washitakiwa na wengine walilazimika kukaa sakafuni ambao walikuja kusikiliza kesi hiyo.

MKUU WA MKOA WA RUKWA NA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU (TFS) WATEMBELEA HIFADHI NA MAPOROMOKO YA LUANJI NA KALAMBO FALLS MKOANI RUKWA



Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls)
Maporomoko ya asili ya Luanji (Luanji Falls) yaliyopo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFS) wakizungumza na wanakijiji wa Kapozwa Wilayani Kalambo juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira yanayowazunguka ukiwemo msitu wa Kalambo na Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yenye urefu wa mita 225.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFS) wakizungumza na wanakijiji wa Kapozwa Wilayani Kalambo juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira yanayowazunguka ukiwemo msitu wa Kalambo na Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yenye urefu wa mita 225.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akionyesha kwa kidole msitu wa hifadhi wa Luanji yanapopatikana maporomoko ya asili ya mto luanji (Luanji Falls). Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na wengine ni Wakala wa Hifadhi ya Misitu Tanzania walipotembelea hifadhi hiyo kwa ajili kuiendeleza. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyeshwa kushangazwa na staili ya nywele ya mmoja ya watoto wa kijiji cha Kapozwa Wilayani Kalambo alipofika katika kijiji hicho na Wakala wa Hifadhi ya Misitu Tanzania kwa ajili ya kuona hifadhi ya Msitu wa Kalambo na maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya katikati waliokaa, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Chima kushoto waliokaa, watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na Wakala wa Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFS) ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

BALOZI WA TANZANIA NCHINI DRC ANTHONY CHECHE AONANA NA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KUJADILI MAHUSIANO YA NCHI HIZO MBILI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongoza kikao kati ya balozi wa Tanzania nchini Congo DRC Balozi Anthony Cheche aliyefika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya kimahusiano kati ya nchi hizo mbili. Mkuu huyo wa Mkoa alimuomba balozi Cheche kunadi fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa pamoja na kuunganisha nguvu ya nchi hizi mbili katika kuwekeza kwenye usafiri wa majini katika Ziwa Tanganyika. Akizungumzia kuhusu wahamiaji haramu amesema ni bora kujenga ushirikiano mzuri wa kibiashara kwa nchi zote mbili ambapo taratibu maalum zitafuatwa kwa wananchi na wafanyabiashara kuingia na kutoka. 
Balozi Anthony Cheche anayoiwakilisha Tanzania nchini DRC akizungumza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo alipoonana na uongozi wa Mkoa kwa lengo la kujitambulisha na kujadili mambo kadhaa ya mahusiano kati ya Tanzania na Congo DRC. Ameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia upya vizuizi vya njiani kwa wafanyabiashara wa nje ikiwemo DRC hususani uwepo wa mizani nyingi barabarani na badala yake ziwepo chache na ziwe mbali kidogo na barabara kuepusha usumbufu kwa wasafiri wengine na wafanyabiashara.
Balozi Anthony Cheche akizungumza katika kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimuonyesha Balozi cheche toleo maalum katika gazeti la Daily News linaloelezea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzinadi kwa wawekezaji nchini Congo DRC.
Baadhi ya wakuu wa idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa wakiteta jambo katika kikao hicho, Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Mipango Ndugu David Kilonzo na Kaimu Katibu Tawala Idar a ya Uchumi na Uwezeshaji Ndugu Respitch Maengo.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiagana na Balozi Anthony Cheche baada kuonana na uongozi wa Mkoa huo mapema leo katika jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...