Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro, wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani), wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu vikiokolewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment