Saturday, February 27, 2016

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU – JUNIOR NATIONAL BASKET ASSOCIATION (JR.NBA


 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya mitoano  Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana,  katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mashabiki wa  Mpira wa kikapu   walio fika katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

YANGA YAIKANDAMIZA CERCALE DE JOACHIM YA MAURITIUS 2-0 UWANJA WA TAIFA

y1
Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia sambamba na mashabiki wao, baada ya kufunga goli la pili dhidi ya timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0. Picha zote na Othman Michuzi.
y2
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akiondoka na mpira na kumuacha Beki wa Timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.

TAFRIJA YA MCHAPALO WA UZINDUZI WA INTANETI YA KASI ZAIDI YA TIGO 4G MKOANI KILIMANJARO YAFANA


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makala(wa pili kulia) akimkabidhi Emmanuel Kilaga, zawadi kutoka Tigo   wakati wa hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Mtaalam wa mtandao kutoka Tigo Samira Baamar.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mtaalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar(wa tatu kulia), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi waliojishindia zawadi mbalimbali.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mjini Moshi juzi

ZIARA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA – MTWARA

kasl1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao  chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao  chuoni hapo , Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl3
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl4
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wafanyakazi wa  kampuni ya TPDC baada ya kuwasili kwenye mtambo wa kuchakata  gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini kukagua shughuli za gesi Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl7
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPDC baada ya kutembelea mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kasl8
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS MPYA WA FIFA NI GIANNI INFANTINO

fi1
Gianni Infantino ndiye aliyechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka duniani Fifa
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
fi2
Infantino akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FIFA
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa mojaWingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .
FI3
Infantino akiwahutubia wajumbe
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fif

UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI WAAHIRISHWA KWA AMRI YA MAHAKA, POLISI WAPAMBANA NA MADIWANI WA UKAWA


Polisi wakipambana na Madiwani wa UKAWA mara baada ya Uchaguzi huo kuairishwa tena leo kutoka na kesi iliyoko mahakamani iliyofunguliwa(Picha kwa hisani ya Fullhabariblog)
sam2
Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiongea na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupata ufumbuzi baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa amri ya mahakama.
sam3 Polisi wakiwa wamekaa kwenye jukwaa la juu wakifuatilia matukio katika uchaguzi huo ambao umeahirishwa kwa amri ya mahakama.
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuairishwa  tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajioi ya kutuliza ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana nakesi iliyoko mahakamani ambapo Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA walipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo
Tukio hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutanga kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi huo kusimamishwa na  mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya  ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo, jambo ambalo ni sawa na kukidi amri halali ya mahakama ya kusimamisha uchaguzi huo kutokana na kesi iliyoko mahakamani
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakaingia  ukumbini humo na kuwataka  madaiwani   hao waachane na zoezi hilo na kuondoka ukumbini,jambo  ambalo liliwachukiza madiwani hao na kuanza vurugu  ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani hao wa Ukawa  ili kuwatoa.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...