Wednesday, February 03, 2016

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI SINGIDA TAYARI KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo, wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mh. Said Amanzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
(PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-SINGIDA)
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu mkoani humo, kushoto ni Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama mbalimbali waliojitokeza kumpokea wakati alipowasili mjini Singida leo.
5
Akina mama na wana CCM mbalimbali wakiimba nyimbo za kumlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili mkoani Singida leo

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...