Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akiwa amembeba mjukuu weke. Kulia ni Zari
MPENZI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ amejifungua mtoto wa kike leo alfajiri saa 10: 40 jijini Dar es Salaam. Mtandao huu umeongea na Meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Salam Sharaf ambaye amethibitisha taarifa hizo na kusema Zari bado yupo hospitali mpaka sasa.
Kutokana na usumbufu aliodai unaweza kutokea, Salam hakuweka wazi hospitali aliyojifungulia Zari. “Ni kweli Zari kajifungua mtoto wa kike majira ya saa 10 alfajiri leo, lakini kutokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sasa siwatajii hospitali aliyojifungulia mpaka hapo baadaye” Alisema Salam. Mtandao huu unatoa pongezi wa Diamond pamoja na Zari kwa kupata mtoto wa kike.
GPL
No comments:
Post a Comment