Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni ‘B’ kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni ‘B’ katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF), akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu ‘B’ wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.
Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni ‘B’ ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji
No comments:
Post a Comment