Thursday, August 27, 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA KITUO CHA WALIOADHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akipewa maelezo ya ujenzi wa kituo cha kuwarekebisha watu walioathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya huko Kidimni Wilaya ya Kati. Anayetioa maelezo hayo (aliyenyoosha mkono) ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. Omar Dad Shajak. Picha na Salmin Said, OMKR.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesifu maendeleo mazuri ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwarekebisha kitabia watu walioingia katika matumizi ya dawa za kulevya kinachojengwa Kidimni Wilaya ya Kati Unguja.


Maalim Seif ameeleza hayo leo wakati alipotembelea ujenzi wa kituo hicho unaofadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao unakisiwa utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.6 na kujengwa na kampuni ya Alhilal ya hapa Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais amewahimiza wasimamizi, wajenzi na mafundi kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo hiyo, ili kuhakikisha jengo hilo linapatikana katika wakati muafaka.

Akitoa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. Omar Dadi Shajak amesema jengo hilo litakapo kamilika litakuwa la ghora tatu na litaweza kutumiwa na watu wapatao 400 wanaume na wanawake.

Amesema vijana watakao kuwepo katika kituo hicho mbali ya kupatiwa matibabu na ushauri wa kuondokana na matumizi ya dawa hizo haramu, pia watapatiwa mafunzo ya ujasiri amali katika karakana itakayo jengwa, ambapo pia kutakuwa na shamba kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya kilimo.

Naye Mwakilishi wa kampuni ya ujenzi ya Alhilal, Hemed Nassor amesema ujenzi wa sehemu ya chini ya jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu, na jengo kamili linatarajiwa kuwa tayari katika kipindi kisichozidi miaka miwili ijayo.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad alifuatana na Waziri wa Nchi wa Ofisi yake, Fatma Abdul Habib Ferej, Katibu Mkuu Dk. Shajak na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Islam Seif Salum.
Khamis Haji, OMKIR

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...