Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni hiyo, Daniel Wadelanga. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Nuebrand EC.
Mjumbe wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba United Bank for Africa, Tesha Filemon (katikati), akizungumza katika mkutano huo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Meneja wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru Idd (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo na matawi yake.
Ofisa Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana na na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment