Monday, August 24, 2015

MKUU WA MKOA MH. JOEL BENDERA AZINDUA MFUKO WA AFYA YA JAMII ULIYOBORESHWA (iCHF ) MKOANI MANYARA

Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkoani Manyara,Mkuu wa Mkoa Mh.Joel Bendera akiwasili katika viwanja vya Halmshauri ya Mji wa Mbulu akiongozana toka kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa –Bw.Ally Uledi, Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe.
Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika moja ya banda la maonyesho ambapo wananchi walipata fursa ya kupimwa afya zao, kuchangia damu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zihusuzo CHF iliyoboreshwa na NHIF.Wengine toka kushoto ni Bw.Isaya Shekifu Kaimu Meneja wa NHIF – Manyara, Bw. Ally Uledi- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Dr.Heri Marwa Mkurugenzi wa Mradi wa Health Insurance – PharmAcess Tanzania.
Mh.Mary Nagu –Waziri katika ofisi ya Raisi Mauhusiano na Uratibu na Mbunge wa Hanang akawaelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na CHF ILIYOBORESHWA katika siku ya uzinduzi .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa shirika la PharmAccess kutoka Uholanzi Bw.Sicco Van Gelder ambao ndio wafadhili wa mradi huu wakishirikiana na NHIF.
Mgeni rasmi wa siku ya uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe kukabidhi moja ya pikipiki tano zilizotolewa kwa maafisa wa CHF iliyoboreshwa ili kuwarahisishia kazi ya uandikishaji na uhamasishaji kwa wananchi wa tarafa tano za wilaya ya Mbulu.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiwasha moja ya pikipiki tano alizokabidhi kwa maafisa wanaoshughulika na CHF ILIYOBORESHWA mbele ya umati wa wananchi wa wilaya ya Mbulu katika siku ya uzinduzi wa mradi huu kimkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Joel Bendera akimkabidhi kadi ya CHF iliyoboreshwa mwanachama mpya aliyejiunga katika siku ya uzinduzi wa kimkoa wilayani Mbulu mkoani Manyara.
 ---
Anna Makange, Mbulu.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Mh. Joel Bendera amezindua rasmi Mfuko wa Afya ya Jamii Uliboreshwa (iCHF) mkoani Manyara.Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mh.Mary Nagu (Mbunge - Hanang) na Waziri katika ofisi ya Raisi Mahusiano na Uratibu, Wakuu wa wilaya za Hanang na Mbulu pamoja Wawakilishi wa wizara ya afya na Ustawi wa Jamii, ulifanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Mbulu. Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri mradi huu na kuhamasisha wananchi wajiunge kwa wingi ili kufanikisha sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote.

Pia halmshauri za wilaya mkoani Manyara zimetakiwa kuweka bajeti maalum itakayowezesha utekelezaji wa mpango endelevu wa kuziingiza kaya maskini katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kila mwaka ili kuwahakikishia huduma bora za matibabu.

Mradi huo wa iCHF mkoani Manyara unaendeshwa kwa ushirikiano baina shirika la Pharm Access International (PIA) la Uholanzi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na Halmashauri za wilaya za Mbulu, Babati na Hanang kwa lengo la kuboresha huduma na kuhamasisha idadi kubwa ya wananchi kujiunga na mfumo wa kulipia kabla gharama za matibabu ili kuzuia vifo visivyo vya lazima katika jamii.

Bendera alisema ili kuiwezesha serikali kufikia lengo lake la kufikisha huduma bora za afya kwa kila mtanzania kuna umuhimu wa kipekee kwa halmashauri zinazounda mkoa huo kuhakikisha wananchi wote wanajisajili katika iCHF wakiwemo maskini ili nao waweze kuhakikishiwa upatikanaji wa matibabu.

“Kwa kutambua changamoto ya kutokuwepo rasilimali za kutosha katika vituo vya kutolea huduma ndio maana serikali iliamua kuanzisha mfumo huu wa kuchangia kidogo kila mwaka gharama za matibabu kabla ili kumwezesha kila mwananchi kupata matibabu kwa nia ya kuchangia fedha kidogo.”, alisema.

Aidha aliongeza, “Wito wangu kwenu wananchi ni jiandikisheni kwa wingi kwasababu ugonjwa haupigi hodi… kwa upande wa halmashauri hebu anzeni kuweka fedha kwa mpango mtakaokubaliana ili wale maskini nao waweze kusaidiwa kupata matibabu kama wenzao wengine wenye uwezo wa kuchangia”, alisema.

Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugine Mikongoti akizungumza katika uzinduzi huo aliwataka watoa huduma za afya kupitia iCHF kumaliza malalamiko ya wagonjwa kwa kuhakikisha michango yote ya wananchi inatumika ipasavyo kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha kuona thamani halisi ya fedha zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa PIA alisema katika miezi sita kuanza kwa utekelezaji wa iCHF humo idadi ya wananchi wanaojiunga inaongezeka kwa kasi kutokana na kuongezwa kwa idadi ya vituo vya kutolea huduma, maduka ya dawa, ushirikihswaji jamii na uhamasishsaji.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...