Monday, August 31, 2015

CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA


Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.

PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama
wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. 
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na
wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
MAMA
MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati
wa uzinduzi huo. 
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...