Wednesday, August 26, 2015

WASHINDI 35 WAPATIKANA DROO YA PILI YA KAMPENI YA MCHEZA KWAO YA BENKI YA NBC

 Meneja Malipo ya Akaunti za Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya pili ya kampeni ya akaunti za mishahara iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo. Jumla ya washindi 35 walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika akaunti zao ya hadi asilimia 50. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na kulia ni Meneja wa Akaunti Maalumu wa benki hiyo, Deogratius Kibodya. 
Meneja wa Akaunti Maalumu ya Benki ya Taifa ya Biashara(NBC), Deogratius Kibodya (kulia) akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwa’ wakati wa droo ya pili iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.  Jumla ya washindi 35 walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika akaunti zao ya hadi asilimia 50. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na Meneja Malipo ya Akaunti za Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...