Nahodha wa timu ya Alliance Academy Ally Hamisi (kushoto) akikabidhiwa
kombe na Mwenyekiti wa Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA)Bw. Jackson Songora
baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza
upande wa wavulana jana.
Nahodha wa timu ya wasichana ya Marsh Meriany Kimbuya (kushoto)
akikabidhiwa na kombe na Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw.
Emmanuel Raphael baada ya kutwaa ubingwa wa U-17 Airtel Rising Stars
mkoa wa Mwanza upande wa wasichana jana.
TIMU ya wavulana ya Alliance Academy ya jijini Mwanza jana imetwaa
uchampioni wa michuano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Aitel Rising Stars kwa kuwafunga Misungwi Academy 3-1 kwenye uwanja wa
CCM Kirumba.
Kwa upande wa wasichana timu ya Marsh ndio iliyotawazwa mabingwa kwa
kushinda timu ya TSC kwa magoli 3-2 katika mchezo mkali uliovuta hisia
za watamazaji waliojitokeza kushuhuduia mtanange huo.
Akikabidhi vikombe kwa washindi, Mwenyekiti wa soka mkoa wa Mwanza Bw.Jackson Songora amewataka wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha Mwanza vyema kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinatarajiwa
kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21. Songora
alisema kwamba kikosi kilichochaguliwa kitaanza mazoezi Jumamosi.
Naye Meneja masoka wa Airtel kanda ya Ziwa Emmanuel Raphel
alizipongeza timu zote kwa kushiriki na kuwaasa wachezaji kulinda na
kuviendeleza vipaji vyao ambavyo ni hazina kwa taifa. Aliseema lengo
lilikuwa ni kuibua vipaji na kuwaasa vijana ambao hawakuchaguliwa
kutokata tama na badala yake wajinge kufanya vizuri mwakani.
Kukamilika kwa michuano hiyo jijini Mwanza ndio kunafunga pazia la
Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa iliyoanza kutimua vumbi mwezi
uliopita.
Hivi sasa kombaini za mikoa zilizochaguliwa kuwakilisha mikoa yao
zinajiandaa kwa fainali za taifa na mwenyekiti wa soka la vijana wa
shirikisho la mpira nchini Bw. Ayoub Nyenzi amesema kuwa maandalizi ya
michuano hiyo yamekamilika.
Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha
mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha
inatarajiwa kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa
kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11
hadi 21.
No comments:
Post a Comment