Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 pamoja na Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015. Kampeni za Uchaguzi huanza siku moja baada ya uteuzi na huisha siku moja kabla ya siku ya kupiga Kura.
Kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa Kampeni zinafuata muda, Kanuni ya 39 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge pamoja na Maadili ya Uchaguzi kifungu cha 2.1 (c) inaelezwa Mikutano yote ya Kampeni itaanza saa 2:00 asubuhi n kuisha saa 12:00 jioni.
Kanuni ya 40 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inasema, Mkurugenzi wa Uchaguzi kabla Kampeni za Uchaguzi wa Rais hazijaanza atavitaka vyama vya Siasa kuwasilisha mapendekezo ya ratiba za Mikutano ya Kampeni, na kanuni ndogo ya (3) inasema, lazima Chama kiwasilishe mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ikionesha tarehe, muda, Mkoa na Wilaya ambapo Mkutano utafanyika.
Aidha, kanuni ya 41 (1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015 inaeleza kuwa iwapo Chama cha Siasa kitahitaji kufanya mabadiliko ratiba au eneo la Mkutano wa Kampeni, kitawasilisha mapendekezo yakiambatishwa na sababu za kutaka kufanya mabadiliko kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambaye kabla ya kufanya marekebisho katika Ratiba husika ataitisha Mkutano wa Kamati ya Kuratibu Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi wa Rais inayojumuisha vyama vyote vyenye wagombea katika nafasi hiyo ili vikubali au kukataa mabadiliko yanayopendekezwa.
Kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni tajwa hapo juu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivialika Vyama vya Siasa vyenye Wagombea wa kiti cha Rais kuwasilisha mapendekezo ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni ya Rais. Mnamo tarehe 22
1
No comments:
Post a Comment