Sunday, August 30, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:NITAUNDA MAHAKAMA MAALUM YA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UFISADI NA UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA

01

Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Njombe katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba wa CCM mjini  humo, Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo huku akiahidi kuboresha mambo mbalimbali katika serikali yake ikiwemo Elimu, Kilimo, Viwanda.
Ameongeza kwamba watu wengi watajiuliza na kusema hizi ni siasa fedha atapata wapi? ” Mimi si mwanasiasa ila ni mtendaji zaidi na ninajua mianya inayopoteza fedha za serikali  nipeni kazi nikazibe mianya hiyo” Amesema wakuu wa idara mbalimbali za serikali wajiandae na kujiweka sawa kabla hajaapishwa kwani hatavumilia uzembe kazini, Wizi na Ufisadi huku akiahidi kuanzisha mahakama maalum itakayoshughulikia kesi za ufisadi na ubadhirifu wa mali za serikalini ili watuhumiwa wahukumiwe haraka.
Uchaguzi mkuu wa jamhuri ya muungano ya Tanzania  wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini Kote. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-NJOMBE)
1
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo.
2
Umati uliohudhuria katika mkutano huo.
3
Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akimnadi Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
4
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa pamoja na wananchi waliohudhuria katika mkutano wake wa kampeni mjini Njombe jana.
5
Wananchi wakipunga mikono yao juu kama ishara ya kumkubali Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
7
Mgombea ubunge wa jimbo la Njombe Kusini: Edward Mwalongo akijinadi mbele ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli.
8
Mabasi maalum yaliyopambwa picha za Dr. John {ombe Magufuli.
9
Mlemavu huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja alikuwa ni miongozi mwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
10
Mgombea ubunge wa jimbo la Kyela mkoani Mbeya Dr. Harrison Mwakyembe akimnadi Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Njombe katika uwanja wa Nanenane.
11
Shilole akikamu jukwaani kaazi kwelikweli.
1213
Kada wa CCM aliyekuwa mjumbe wa bunge maalum la Katiba akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Njombe Jana.
14
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mh. Temba akifanya vitu vyake jukwaani.
15
Chege naye amekonga nyoyo za wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
16
Mama Martina Jonas wa Njombe akiwa na watoto wake ambao ni watumishi wa CCM  kulia Edward Mpogolo na kushoto Rodrick Mpogolo wakati alipohudhuria katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Njombe
17
Vijana waendesha Bodaboda wakipiga vuvuzela wakimshangilia  Dr. John Pombe Magufuli.
18
Wana CCM wakishangilia.
19
Msafara wa Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Nanenane.
20
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wakati akiwa njiani kuelekeamjini Njombe kwa ajili mkutano wa kampeni.
21
Akina mama wakimpokea kwa matawi ya miti huku wakicheza ngoma.
22
Wananchi wakimpokea kwa mabando yenye kumsifu Dr. John Pombe Magufuli.
23
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe.
24
Vikongwe hawa ambao majina yao hayakufahamika wanaonekana wakijadili jambo wakati wa mkutano wa kampeni wa Dr. John Pombe Magufuli katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe.
25
Wananchi hawa wakifurahia hotuba ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kupitia Chama Chama Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Ilovi Wanging’ombe mkoani Njombe.
26
Hawa wakifuatilia mkutano huo.
27

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...