Tuesday, August 25, 2015

FAIDA BENKI YA EXIM YAKUA KWA ASILIMIA 69

 Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kushoto) na Meneja Mwanadamizi wa utafiti na uchambuzi wa biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Mrawa (wa kwanza  kulia)
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (wa kwanza kulia)akisisitiza jambo  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (katikati) na  Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde

Benki ya Exim Tanzania imefanikiwa kujipatia faida ya sh. bilioni 12.79 (kabla ya kodi) katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu, takwimu zinazoonyesha ongezeko la faida kwa asilimia 69 katika benki hiyo.

“Ongezeko hilo ni kubwa ikilinganishwa na faida yash.bilioni 7.56 tuliyoiopata katika robo mwaka iliyotangulia na hivyo basi tunajisikia fahari kutangaza faida hii mbele yenu,’’ alibainisha Afisa Fedha Mkuu wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Bw Ponda faida hiyo pia ni sawa ongezeko la asilimia 28 ikilinganishwa na faida ya kiasi cha sh. bilioni 13.96 katika kipindi cha miezi sita kwa mwaka uliopita.

 “Katika robo mwaka hii iliyoisha mwezi Juni, jumla ya mapato kwenye faida  itokanayo na riba ilikuwa kwa asilimia 26 hadi kufikia sh. bilioni 17.9  ongezeko lilichangiwa na gharama nafuu ya amana zetu sambamba na usimamizi bora wa fedha,’’ alibainisha.

Zaidi Bw. Ponda alisema katika kipindi hicho  faida isiyotokana na riba ilikuwa kwa asilimia 43 hadi kufikia kiasi cha sh. bilioni 12.3 kutoka sh. bilioni 8.6 iliyorekodiwa katika mwaka uliopita.

Benki hiyo pia ilikuwa na mapato mgao kutokana na uwekezaji wenye ukubwa kiasi cha sh. bilioni 2.3 ikilinganishwa na kiasi cha sh. bilioni 2 kilichorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

"Nguvu ya ukuaji wa mapato inaoyesha mafanikio ya Benki.. Tunaendelea kuboresha  ufanisi katika uendeshaji na utoaji wa huduma zetu ili kuwaridhisha zaidi wateja wetu. Kwa ripoti hii  matokeo yanaonyesha kwamba Exim tumeonyesha utendaji bora hasa kwa kuhusisha rasilimali watu na technolojia iliyo bora zaidi "aliongeza.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...