Monday, August 24, 2015

UN KUBORESHA VYOO VYA SHULE 10 KILIMANJARO

IMG_4176Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na walimu mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Kiboriloni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kuweka msingi kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo. Kulia kwake ni Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa nchini, yatasaidia kuboresha vyoo katika shule 10 zilizopo katika manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.
Hayo yalisemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya choo katika shule ya msingi Kiboriloni.
Alisema pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka watoto kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.
Aidha aliwataka wanafunzi kuhakikisha kwamba wanajenga mshikamano mkubwa na wenye upendo kila kundi likithamini kundi jingine kwa ajili ya ustawi wa taifa .
Alisema wasichana kwa wavulana kuheshimiana kwani katika hilo wataweza kutengeneza taifa linaloheshimiana na hivyo kulinda msingi wa maisha wa amani unaowezesha maendeleo na ustawi wa jamii.
Aliwataka wanafunzi hao kushikilia ndoto zao na kusaidia kutambua kwamba wanahitajika kutunza mazingira na kujali afya zao. Continue reading →

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...