Wanachama wa Chadema wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wakiandamana kupinga maamuzi ya chama hicho kukata jina la mshindi wa kura za maoni na kumteua aliyeshindwa ,mbali ya kuandamana pia wanachama hao zaidi ya 500 walikihama chama hicho na kujiunga na ACT Wazalendo.
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya chama wilaya walikokwenda kurudisha kadi kabla ya kuhamia ACT wazalendo.
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya ACT Wazalendo ambako walifika kuomba kujiunga huko.
Wanachadema wakirudisha kadi za chamna hicho na kujiunga na ACT wazalendo.
Kadi zikiwa zimekusanywa kwa kuchomwa moto.
Hivi ndivyo kadi zinavyoteketezwa kwa moto baada ya wana Chadema kujiengua na chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo.
No comments:
Post a Comment