Thursday, August 27, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:NINASIMAMIA NINACHOKIAMINI, NATAKA TANZANIA YENYE MABADILIKO BORA SIYO BORA MABADILIKO

????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli kiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya leo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Tunduma na kuhudhuriwa maelfu ya wananchi, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Tunduma kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania katika kupeleka gurudumu la maendeleo mbele zaidi.
Amesema ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa akisimamia kile anachokiamini kwamba ndiyo maendeleo ya watanzania, amekuwa mkweli, muaminifu kwa viongozi wake, mcha mungu na mchapa kazi hivyo anaomba nafasi ya urais ili aweze kuona Tanzania yenye mabadiliko bora kwa watanzania na siyo bora mabadiliko.
Uchaguzi mkuu wa jamhuri ya Muungao ya Tanzania wa Rais , Wabunge na Madiwani  unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-TUNDUMA)
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya leo.
????????????????????????????????????
Uwanja wa shule ya msingi Tunduma ukiwa umefurika wananchi waliokuja kumsikiliza mgombea urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na udiwani katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tunduma leo.
????????????????????????????????????
Machifu wa Momba wakimuombea Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tumduma leo.
????????????????????????????????????
Wilayani Ileje katika mji wa Katumba mabango yanayoonyesha picha za Dr. John Pombe Magufuli tu.
????????????????????????????????????
Askari wa Usalama Barabarani akiongoza msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye uwanja wa mkutano mjini Katumba.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadimgombea ubunge wa jimbo la Ileje Mh. Janet Mbene katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini .
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na Mzee Gideon Cheyo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ileje na Waziri wa Ardhi na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipunga mkoano kama ishara ya kuwasalimia wananchi wakati alipowasili kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Vywawa wilayani Mbozi.
????????????????????????????????????
Wasanii ni miongozi mwa wananchi wanaojitokeza katika mikutano ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli .
????????????????????????????????????
?
Mgombea udiwania wa kata ya Ilolo akijinadi mbele ya wananchi katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwasalimia viongozi mbalimbali wa dini mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni mjini Vwawa.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya na mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi akimkaribisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli ili aongee na wananchi mjini Tunduma.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwapungia mkoni wananchi wakati alipowasili mjini Tunduma.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akipokelewa kwa mbwembwe katika mji wa Ndalambo akiwa njiani Kuelekea mjini Tunduma.
????????????????????????????????????
Dogo huyu hakukubali mpaka alipomuona Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli  katika kijiji cha Luasho wilayani Mbomba.
????????????????????????????????????
Vijana wa chama cha CHADEMA wakimshangaa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli hayupo pichani wakati alipowasili katika kijiji cha Ndalambo.
????????????????????????????????????
Magufuli jamani Jembe na Nyundo viligeuka ngoma wakati alipokuwa akipokelewa na wananchi katika kijiji cha Ndalambo akiwa njiani kuelekea Tunduma wilayani Momba.
????????????????????????????????????
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndalambo.
????????????????????????????????????
Picha ya Magufuli ilikuwa muhimu sana kwa mtoto huyu ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika kijiji cha Nzoka wilayani Momba.
????????????????????????????????????
Askari polisi akiimarisha ulinzi katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Nzoka.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli, akifanya maombi na watawa Christina na Emiliciana wa kanisa Katoliki katika mji wa Laela mara baada ya mkutano wake katika mji wa Laela akiwa njiani kuelekea Tunduma na Ileje kuendelea na kampeni zake za kuingia Ikulu, Katikati ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mh. William Lukuvi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimsalimia Bw. Joseph ambaye ni mlemavu wa viungo mara baada ya mkutano wake katika mji wa Laela mkoani Rukwa leo asubuhi.,
????????????????????????????????????
Bw. Joseph ambaye ni mlemavu wa viungo akinyoosha mkono  kumsalimia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mji wa Laela akiwa njiani kuelekea Momba, Mbozi na Ileje.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwapa maagizo wagombea udiwani katika mji wa Laela ili wamletee yeye ahadi yoyote watakayoahidi kuwatekelezea wananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...