Friday, August 28, 2015

LOWASSA AHUTUBIA BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA JIJINI DAR

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono baadhi ya Wanawake wanachama wa CHADEMA, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee akizungumza na Umati wa Kinamama wa Chama hicho, uliokuwa umefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza hilo, uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).
Wakinamama hao wakimshangilia Mh. Lowassa na Babu Duni wakati walipowasili Ukumbini hapo.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akiwasalimia kina mama hao ambao walikosa nafasi ndani ya Ukumbi na kuamua kukaa nje.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia kina mama hao.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza machache wakati akiwasalimia maelfu ya Wanawake wanaounda Baraza la BAWICHA, waliokuwa wamekaa nje ya jengo la LAPF kutokana na kukosa nafasi ndani ya Ukumbi huo. Mh. Lowassa alilazimika kusimama na kuwasalimia kinamama hao kabla ya kuingia Ukumbini kulihutubia Baraza hilo.
Mh. Lowassa na Ujumbe wake wakiwasili Ukumbini.
Salam kwa Wajumbe.
Baadhi ya Wadau wa Sanaa ya Filamu nchini waliokuwepo kwenye Mkutano huo wa BAWICHA.
Shangwe Ukumbini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiteta jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mwenza, Dkt. Juma Haji Duni, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Uliofanyika jana Agosti 27, 2015.
Mmoja wa Kinamama wanaowakilisha Watu wenye ulemavu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee  akifatilia Hotuba ya Mama anaewakilisha Watu wenye Ulemavu.
Viongozi wa Kuu.
Mmoja wa Wasanii wa Filamu nchini, Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea Keki ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutoka kwa Msanii wa Filamu nchini, Aunt Ezekiel.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimpongeza Msanii wa Filamu nchini,  Jacqueline Wolper.
 Jacqueline Wolper akizungumza kwa niaba ya wenzake.
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya Wanawake wa Chama hicho waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015, wakati wa Mkutano wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWICHA).

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...