Wednesday, August 26, 2015

DR. JOHN POMBE MAGUFULI:WATENDAJI WAZEMBE NA WABADHIRIFU WAJIANDAE KUFUKUZWA KAZI

????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mjini Sumbawanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye uwanja wa Nelson Mandela mkutano ambao umehudhuriwa na maelfu ya wananchi waliokuja kumsikiliza mgombea huyo mwenye misimamo thabiti katika utekelezaji  wa majukumu yake.
Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo yeye pamoja na wabunge na madiwani wa CCM ifikapo Oktoba 25 mwaka huu  ili aweze kufanya kazi na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kuwaletea maendeleo watanzania bila kubagua itikadi zao za kisiasa, Dini na Makabila yao.
Amewataka watendaji wa serikali wazembe na wabadhirifu wa mali ya umma kujiandaa kufukuzwa kazi endapo hawatakwenda na kasi yake katika kuwatekelezea mambo muhimu ya maisha na maendeleo kwa ujumla wananchi walio wanyonge. Amesema anajua wapi zinapovujia fedha za serikali hivyo atahakikisha anaziba mianya hiyo ili serikali ipate mapato yake kikamilifu na kuwafanya watoto wa watanzania wanyonge waliowengi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na hilo linawezekana.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SUMBAWANGA)
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mjini Sumbawanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye uwanja wa Nelson Mandela
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano  mkubwa wa kampeni wa mgombea wa urais kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mjini Sumbawanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye uwanja wa Nelson Mandela
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga Mh. Aeshi Hilaly  mjini kwa  wananchi wa mjini Sumbawanga katika  mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye uwanja wa Nelson Mandela
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Sumbawanga katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jana.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga wakati alipomnadi Dr. John Pombe Magufuli mgombea urais wa Tanzania.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimshukuru Mh. Mizengo Pinda Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  mara baada ya kumtambulisha kwa wananchi katika mkutano wa Kampeni uliofanyika mjini Sumbawanga jana.
????????????????????????????????????
Mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga Mh. Aeshi Hilaly akiwahutubia wananchi wa mjini Sumbawanga na kuwaomba kura za ndiyo katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 25h mwaka huu.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa kampeni mjini Sumbawanga.
????????????????????????????????????
13
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika mkutano wa kampeni uliofanyika Majimoto Kibaoni mkoani Katavi jana.
15
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiongozwa na Mjumbe wa Kamati kuu  Mh. Mizengo Pinda huku akipungia  mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la Majimoto Kibaoni wilayani Nsimbo mkoani Katavi jana.
16
Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu William Lukuvi akiwatunza wapiga ngoma wakati wa mapokezi ya mgombea urais Dr. John Pombe Magufuli wakati alipowasili katika eneo la Majimoto Kibaoni mkoani Katavi.
17
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika eneo la Majimoto Kibaoni mkoani Katavi kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Mh. Mizengo Pinda na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi.
18
Wananchi wakinyanyua mikon yao juu kuashiria kumkubali Dr. John Pombe Magufuli.
19
Magufuli tuu 
20
Vijana wakifuatilia hotuba ya Dr. John Pombe Magufuli.
21
Wakifurahia hotuba ya Dr. John Pombe Magufuli wakati akisalimia wananchi katika kata ya Matai akiwa njiani kuelekea Kalambo.
23
Wasanii wa ngoma za asili nao wakifuatilia hotuba ya Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Namanyere wilayani Nkasi.
24
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimsalimia mama mzazi wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mh. Mizengo Pinda mama Albertina Kasanga miaka 86 wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kibaoni jana katikati  ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mh Mizengo Pinda na kushoto ni Mama Tunu Pinda.
25
Magufuli hoyeee!! 
28
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Nkasi Mh Ally Kessy wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Namanyere mkoani Rukwa jana.
30
Kada wa Chama cha Mapinduzi Chrisant Mzindakaya akimuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga jana.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...