MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam jana asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015.
Dovutwa amekuwa mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho.
MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akikabidhiwa fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, kutoka kwa afisa uchaguzi mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC jijini Dar es Salaam jana Jumamosi Agosti 1, 2015.
Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment