Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya kikazi ya siku 9 mkoani Dodoma akizna na wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na wilaya zingine na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kulia katika picha ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MPWAPWA).Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa mara baada ya kukabidhi orodha hiyo ya wadaiwa sugu wa bili za maji kwa Mkuu wa mkoa wa Galawa ambaye anaonekana akiipitia orodha hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mfereji wakati alipokuwa akivuka mfereji huo akielekea akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege Mpwapwa huku akiwa ameongozana na Bi Anna Mlewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma , Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa wa pili kutoka kushoto na, wengine anayefuata ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam KimbisaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka mara baada ya kushiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga mfereji wa maji katika shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga kijiji cha Msagali.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mazae kata ya Kisokwe kushiriki ujenzi wa zahanati.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la bweni katika shule ya sekondari ya Mpwapwa lililoungua ambapo pia ameshiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni hilo.Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mh. Adam Kimbisa akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni hilo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hiku Galawa wakishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni la shule ya sekondari ya Mpwapwa lililoungua moto na kuteketeza mali zote za wanafunzi.Mkuu wa mkoa wa Dodoma akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanausalama katika msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa ngoma wakati alipowasili katika kijiji cha Berege na kusalimia wananchi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mpwapwa mara baada ya kukagua bweni lililoungua kwa moto katika shule hiyo.Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mpwapwa.Mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni mstaafu Chiku Galawa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mpwapwa.Umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo.Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa.
No comments:
Post a Comment