Thursday, March 05, 2015

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME YA REA MKOANI DODOMA

1
Mtaalam kutoka kampuni ya kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Azizi Msuya (kushoto) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa Dodoma katika eneo iliyopo bohari ya kuhifadhi vifaa vya ujenzi vya kampuni hiyo, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kamati hiyo inafanya ziara kwenye miradi ya umeme mkoani Dodoma lengo likiwa ni kujionea utekelezwaji wake   pamoja na kuzungumza na wawakilishi wa wananchi.
2
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (kushoto) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya umeme katika kijiji cha Msanga kilichopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
3
Mtaalam kutoka kampuni ya kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Azizi Msuya (wa pili kutoka kushoto) akielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa katika usambazaji wa miundombinu ya umeme katika eneo la Kibaigwa wilayani Kongwa mkoani Dodoma. Kamati hiyo iliiagiza kampuni hiyo kuweka miundombinu ya umeme katika vijiji vilivyosahaulika.
4
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chambani- Pemba, Yusuph Salim (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
6
Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dodoma, Zakayo Temu ( wa pili kutoka kulia) akielezea mikakati ya shirika hilo katika usimamizi wa miradi inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
8
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Geita, Josephine Chagula ( wa tatu kutoka kulia) akitoa ushauri kwa kampuni ya kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wa namna ya kuboresha kasi ya usambazaji wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa Dodoma.
9
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa, Murtaza Mangungu (katikati) akilishauri Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) namna bora ya kuwawezesha wananchi kuunganishiwa na huduma ya umeme mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...