Monday, March 23, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA MKOA WA KILIMANJARO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatisha kwenye migomba alipokuwa akikagua mifereji ya inayotiririsha maji kuelekea kwenye mashamba ya ndizi akiongozana na Mh. Agrey Mwanri.

Akielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri amesema ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa ambapo vijiji vyote katika jimbo hilo vina maji safi na salama ya kunywa, Umeme umefika katika vijiji vyote kinachondelelea ni usambazaji kwa kila mwananchi, Suala la huduma za afya nalo liko vizuri kwani vimejenga vituo vya afya karibu kila maeneo na baadhi ya zahanati zinamaliziwa kujengwa.
Suala la Elimu wakati mbunge huyo akiinga madarakani Siha kulikuwa na sekondari moja, lakini sasa kuna sekondari 17 na ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa kiwangi cha juu, Maabara zinakamilishwa ambapo mabati yamesambazwa karibu kila shule ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo.
Akizungumza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM amemsifu Mh. Agrey Mwanri kwa kazi aliyoifanya katika jimbo hilo kwa kufanya kazi vizuri na kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaambia wananchi katika mkutano huo kwamba kama kiongozi anafanya kazi nzuri hakuna haja ya kubadilisha viongozi kama mashati, Mwacheni awaleteeni maendeleo.
Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape nnauye Katubu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye chumba cha maabara cha hospitali ya wilaya Siha mara baada ya kuyakagua magari matatu ya kubebea wagonjwa.
Sehemu ya jengo la hospitali hiyo ya wilaya ya Siha kama lionekanavyo pichani,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Siha, kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndugu Oscar Temu.
 Ndugu Kinana akitoka nje ya ofisi hiyo mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kuikagua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya wilaya ya CCM Siha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...