Friday, March 27, 2015

MKUTANO WA KAMATI YA WATALAAM WA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA KAMISHENI YA UCHUMI YA AFRIKA (ECA) WAANZA ADDIS ABABA – ETHIOPIA.

1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamis H. Mwinyimvua (Kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mh.Naimi Azizi wakiwaa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Watalaamu wa masuala ya Fedha Afrika unaofanyika Mjini Addis Ababa – Ethiopia.
2
Baadhi ya wajumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 8 wa Watalaam wa masuala ya Fedha – Afrika wakijadili jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa ‘United Conference Centre’ Addis Ababa. Kulia ni Nd.Mbayani Saruni na Kushoto ni Bi.Glory Sindilo.
3
Mh.Naimi Azizi Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia (Katikati) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) wakifurahia jambo na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 8 wa Watalaamu wa masuala ya Fedha wa Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.
……………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Tanzania inashiriki mkutano wa nane wa Wataalamu wa Fedha, Uchumi na Mipango kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA) umeanza nchini Ethiopia kwa kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa watalaamu ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Afrika ambao utafanyika kuanzia Machi 30 hadi 31 mwaka huu Addis Ababa nchini Ethiopia.
Katika Ufunguzi wa Mkuatano huo Mh. Abraham Tekeste,Waziri wa Fedha na Uchumi wa Ethiopia alisisitiza kuwa umakini unatakiwa katika utekelezaji wa sera tulizojiwekea, vipaumbele na mikakati ya maendeleo ya kifedha kabla ya kikao cha malengo ya maendeleo endelevu kitakachofanyika Septemba ,2015.
Mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine utajadili kanuni na utaratibu wa kamati ya watalaam wa masuala ya fedha, Uchumi na Maendeleo na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Afrika, utatanguliwa na uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya wataalam na kamati ya Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa nchi wanachama wa AU, na ECA.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...