Meneja Masoko wa CFAO Motors ltd. Sheikha Said (wa pili kulia) akitoa maelezo ya vijarida vya matoleo mapya ya magari aina ya Mercedes Benz kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto). Kulia ni Sales Representative wa CFAO Motors Ltd. Edwick Mwamba.
Sales Representative wa Kampuni ya CFAO Motors Ltd. Edwick Mwamba akizungumza jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) alipotembelea meza ya Mercedes Benz magari yanayouzwa na kampuni ya CFAO Motors.
Wageni waalikwa kwenye #MBAR2015 Eleganza Fashion show wakipitia majarida mbalimbali yenye taarifa za magari aina ya Mercedes Benz.
‘Model’ wa kiume, kike watia fora na mavazi ya ubunifu ‘run way’ yabamba ndani ya dakika 20.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Ile shoo maalum ya mwaka iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa hatimaye usiku wa Machi 21 ndani ya Serena Hotel jijini Dar es Salaam, shoo hiyo ‘Mercedes Benz Ally Remtullah 2015 Eleganza’ imeweza kuwa ya aina yake na ya kipekee kwa kuvutia kila mmoja aliyehudhuria shoo hiyo.
Kama kawaida yake mbunifu wa mavazi, Ally Remtullah amekuwa akifanya vizuri kila mwaka kwenye shoo zake hizo anazoziandaa ambapo kwa shoo ya mwaka huu imezidi kuingia kwenye historia kwa kuonyesha toleo jipya ‘New collection 2015’.
Miongoni mwa mambo yaliyoweza kubamba katika shoo hiyo ni pamoja na jukwaa ‘Run way’ kwa Models hao kulitendea haki na na kuonekana tukio la Kimataifa.
Ni dhahiri shoo hiyo kwa kila aliyeshuhudia asilimia 100, ni ya Kimataifa. Ambapo ilichukua ndani ya dakika 20 huku kila Model akipangilia vilivyo na mavazi maalum hali iliyopelekea kuliteka jukwaa.
Aidha, kwa upande wake Ally Remtullah alipongeza wadau wote kwa kuendelea kumuunga mkono ambapo aliiambia Modewji blog kuwa baada ya hapo anatarajia kuendelea kufanya maonyesho zaidi ikiwemo ndani na nje ya nchi.
Pia aliwashukuru wadhamini akiwemo mdhamini Mkuu, Kampuni ya CFAO Motors LTD wauzaji wa magari kupitia brand yake ya Mercedes Benz. Wengine ni MeTL Group kupitia bidhaa za ki-elekroniki za LG na wengine wengi.
Fuatana na camera ya modewji blog kwa picha za ‘Cat walk’ ndani ya hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Hi Mr. Photographer…..Greetings from Abby Plaatjes.
round of applause for Ally Rehmtullah…..
Here comes Ally Rehmtullah….. Yeeeeeh.
Model tatu tofauti za magari aina ya Mercedes Benz.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakitoka kwenye ukumbi wa Marquee ndani ya hoteli ya Serena mara baada ya kumalizika Fashion show ya #MBAR2015 Eleganza.
No comments:
Post a Comment