Tuesday, March 31, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUU WA SITA WA BARAZA LA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI (IUCEA) JIJINI DAR ES SALAAM.

 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki, waratibu wa mkutano Mkuu wa Sita wa majadiliano ya kukuza maendeleo endelevu ya mifumo ya Elimu ya Juu na Maendeleo ya Kiuchumi. Mkutano huo ulifunguliwa leo Machi 31, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
1
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi mkutano Mkuu wa Sita wa majadiliano wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) wenye lengo la kukuza maendeleo endelevu ya mifumo ya Elimu ya Juu na Maendeleo ya Kiuchumi, uliofanyika leo Machi 31, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
34
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, baada ya kuufungua ramsi, leo Machi 31, 2015.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Picha na OMR

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...