Kinana amewaasa wana CCM kukemea vitendo vibaya vya viongozi wa serikali na watendaji wanaokiuka utaratibu wa kazi na kufanya mambo yasiyokuwa ya kimaadili katika utendaji wao. Ili kukiweka chama hicho katika sura nzuri kwa wananchi, “Wana CCM tunatakiwa kuwa wa kwanza kukemea maovu siyo wana CCM tunaanza kuwalinda na kuwatetea waovu jambo ambalo si sawa kabisa, Tutahakikisha tunairudisha CCM ya wanyonge na masikini watoto wa wakulima na wafanyakazi aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere”, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-HAI-KILIMANJARO)
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na wana CCM wa wilaya ya Hai mara baada ya mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wa mkoa wa Kilimanjari wakishiriki kuchimba msingi wa jengo la darasa wakati aliposhiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Modio Masama Mashariki wilayani Hai.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijulia hali Mzee Israel Elly Nawinga aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa miaka ya nyuma nyumbani kwake Masama Mashariki, wa kwanza Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama na katikati ni Mkuu wilaya ya Hai Ndugu Anthony Mtaka.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijulia hali Mzee Israel Elly Nawinga aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa miaka ya nyuma nyumbani kwake Masama Mashariki, Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Hai Ndugu Anthony Mtaka.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama akimsalimia Mzee Israel Elly Nawinga aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa miaka ya nyuma nyumbani kwake Masama Mashariki, wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipomtembelea nyumbani kwake Masama Mashariki wilaya i Hai.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua daraja la Mnepo kijiji cha Kiyungi wilayani Hai lililojengwa na serikali.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi katika kingo za daraja la Mnepo kijiji cha Kiyungi wilayani Hai lililojengwa na serikali wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo..Daraja la Mnepo katika kijiji cha Kiyungi likiwa katika hatua mbalimbali za ujenziKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka katika daraja la awali lililokuwa likitumiwa na wananchi ambapo wananchi hao wamesema watu wengi wamepoteza maisha na kuumia wakati wakivuka daraja hilo kwa kipindi chote ambacho kulikuwa hakuna daraja imara na la kudumu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka katika daraja hilo.Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Hai wakiwa katika mkutano mjini Boma Ng’ombe.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika kutano wa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Hai.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi wa kijiji cha Mtakuja ambacho wakazi wake na majirani zao wana mgogoro mkubwa wa mipaka ya ardhi na kiwanja cha ndege cha KIA mkoani Kilimanjaro.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi hao mara baada ya kuwasili kijijini hapo.Wananchi hao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja wilayani Hai.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzana wauguzi na madaktari wakati alipotembelea katika hospitali ya wilaya ya hai mkoani Kilimanjaro.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizunguma na wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua baadhi ya mashine katika chumba cha miozni hospitalini hapo.Nape Nnauye akifanyiwa vipimo katika chumba cha mionzi hospitalini hapo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na madaktari na wauguzi pamoja na watumishi wengine wa hospitali hiyo.Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Snow View Boma Ng’ombe wilayani Hai.Mamia ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Snow View Boma Ng’ombe wilayani Hai.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo.Kikundi cha vijana kikiimba wimbo maalum katika mkutano huo.Madereva wetu kutoka kulia ni Mick Mzee wa Cremia, Prosper na Adam Soud.
No comments:
Post a Comment