Monday, March 30, 2015

Waziri Lukuvi afanya ziara Shirika la Nyumba la Taifa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu ambaye alikuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu utendaji wa Shirika hilo leo asubuhi. Waziri Lukuvi yuko katika ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa Shirika hilo ambapo leo na kesho atatembelea baadhi ya miradi ya NHC iliyopo jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa NHC.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na James Rhombo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NHC, wakati akikaribishwa Makao Makuu ya NHC. Kulia na Felix Maagi, Hamad Abdallah na Raymondo Mndolwa. 
 Waziri Lukuvi akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio kuingia kwenye ofisi za makao makuu ya NHC leo.
 Waziri Lukuvi akisalimiana na Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, wakati akikaribishwa Makao Makuu ya NHC. Kulia kwa Maagi ni James Rhombo, Hamad Abdallah na Raymondo Mndolwa. 
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa Shirika la NYumba la Taifa Raymond Mndolwa, akimsindikiza Waziri Lukuvi kuingia ukumbini NHC ambapo alipata fursa ya kuwasalimia wafanyakazi wa shirika hilo.
 Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC
 Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC

 Wakurugenzi wa NHC
 Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)

Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)

 Waziri Lukuvi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC
 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NHC katika picha.



No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...