Saturday, March 07, 2015

SERIKALI YA JAPAN YAIPATIA MSAADA WA DOLA LAKI 1.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki Jijini Dar es salaam,kulikofanyika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) akionyesha kitu kwenye karatasi kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja Mbunge wa Viti Maalum – Monduli,Mh. Namelock Sokoine,wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga akitoa hotuba yake mbele ya Ujumbe wa Wilaya ya Monduli pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakisaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Monduli.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.Wengine pichani ni Mbunge wa Viti Maalum – Monduli,Mh. Namelock Sokoine (katikati),Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Idara ya Miradi wa Ubalozi wa Japan nchini,Takashi Higuchi.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakibadilishana mikataba mara baada ya kuisaini,wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika leo nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki jijini Dar.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri ya Monduli dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi miwili ya wilaya hiyo.Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) Mbunge wa Viti Maalum – Monduli,Mh. Namelock Sokoine pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum – Monduli,Mh. Namelock Sokoine akitoa akizungumza machache mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha ya pamoja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga mara baada ya hafla hiyo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...