Friday, March 27, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE SAME MAGHARIBI, KESHO KUENDELEA SAME MASHARIKI

3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kama chifu wa wapare mara baada ya kupokelewa na wananchi katika kijiji cha Njoro  jimbo la Same magharibi.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati alipowasalimia katika kijiji cha Makanya Same.5Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mh. David Mathayo David akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Gonjamza Suji wilayani Same.Wana6Wananchi wakinyanyua mikono yao juu huku wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipowasili katika kijiji cha Suji.7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Suji8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki katika kazi ya kufukia mabomba ya mradi wa maji katika kijiji cha Gonjaga Suji wilayani Same.9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Suji  anaoshirikiana nao kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David.10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David wakishiriki wakifungua maji ya bomba mara baada ya Kinana kuzindua mradi huo katika kijiji cha Suji wilayani Same.11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi jimboni humo12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro Mh. David Mathayo David katikati na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakijadiliana jambo huku mvua ikinyesha kwenye stendi ya mabasi ya Same , Mvua hiyo ilisababisha kuahirishwa kwa mkutano huo na kupangwa kufanywa baada ya wiki nne.13Wana CCM wakiimba nyinbo za kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huo mjini Same.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...