Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akijibu swali la Mhe.Haroub Shamis Mbunge wa jimbo la Chonga kuhusu jinsi gani serikali inawasaidia waadishi kuandika habari za kibiashara,Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene akijibu swali la Mhe.Philipa Mturano Mbunge wa viti maalum lililokuwa likihoji ni namna gani Serikali imejipanga kuthibiti biashara ya vyuma chakavu kutokana na kuwepo na wizi wa mabomba.
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe.Gaudensia Kabaka akisoma muswada wa sheria ya Udhibiti wa Ajira kwa Wageni ya mwaka 2014 kwa mara ya pili ndani ya Bunge, tarehe 18/03/2015 Mjini,Dodoma.
Mhe.Victor Kawawa akichangia hoja juu ya Muswada wa sheria ya udhibiti wa Ajira za wageni wa mwaka 2014 uliyosomwa na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka,tarehe 18/03/2015 bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (kushoto) akizungumza na Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kikao, Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment