Thursday, March 26, 2015

BUNGE LA SOMA MUSWADA WA UDHIBITI MADAWA YA KULEVYA

1
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe.Jenista Mhagama akisoma Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya wa Mwaka 2014,Mjini Dodoma tarehe 24/03/2015
2
Mheshimiwa Neema Hamid Mbunge wa (Viti Maalum) akisoma Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Muswada wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya,Mjini Dodoma tarehe 24/03/2015.
3
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Anne Kilango akijibu swali lililoulizwa na Mhe.Roseweeter Kasilika (Viti Maalum) lilihoji juu ya Serikali kutilia maanani Mwongozo kwa Elimu ya Awali,Mjini Dodoma tarehe 24/03/2015
4
Waziri Mkuu Mhe.Peter Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Amos Makalla ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati kikao cha bunge kinaendelea Mjini Dodoma,tarehe 24/03/2015.
5
Baadhi ya Mawaziri na Wabunge wakiwasili katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kuanza kikao cha Bunge,tarehe 24/03/2015.
6
Mbunge wa Jimbo la Ole (CUF)Mhe.Rajab Mbarouk akichangia hoja katika Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Madawa ya Kulevya,Mjini Dodoma tarehe 24/03/2015.
……………………………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas-MAELEZO,Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe.Jenista Mhagama amesoma Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya wa mwaka 2014 kwa mara pili Bungeni Mjini Dodoma tarehe 24.03.2015.
Mhe.Mhagama alisema kupitia Muswada huu Serikali itaunda chombo kitakachosimamia na kudhibiti biashara ya Madawa ya Kulevya pamoja na kuanzisha vituo vitakavyo toa tiba kwa waadhirika wa madawa ya kulevya. 
“Sehemu ya sita ya Muswada huu unahusu uanzishwaji wa Mfuko wa Udhibiti wa Kupambana na madawa ya kulevya na na pia sehemu tano inahusu kufilisi mali wafanyabiashara za madawa ya kulevya pale wanapitiwa hatiani,hivyo basi sheria hii itaipa meno Mamlaka itakayoundwa kwa ajili ya kupambana nawafanya biashara wa Madawa ya Kulevya pamoja na wahusika wote wanajihusisha na madawa ya kulevya,ikiwa ni pamoja na ujazaji wa fomu kwa watuhumiwa watakao kamatwa katika biashara hizo,”alisema Mhe.Mhagama.
Kwa upande wa maoni ya kambi ya Upinzani inayoshughulikia masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) yaliyosomwa na Mhe.Rajab Mbarouk alisema kambi ya Upinzani inaishauri Serikali kwa ujumla katika vifungu vyake mbalimbali vinavotoa adhabu ya faini viondolewa na badala yake iwe ni kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.
Kwa upande wa uchangia wa maoni kutoka kwa wabunge juu ya muswada huo Mhe.Mwibara Lugola (Mb) CCM aliishauri Serikali kutoa hukumu kwa watakao kamatwa na madawa papo kwa papo kwa mfano mtu alinayekamatwa na madawa ya kulevya akiwa ameyameza au kuyabeba.Pia alisisiitiza kwa kuiomba Serikali iondoe suala la faini na badala yake iwe ni kifungo cha maisha au kunyongwa mpaka kufa.
Aidha,naye Mhe.David Silinde (Mb) alitoa maoni kwa Serikali kwa kuiomba Sheria hii ionyeshe ni namna gani itadhibiti suala la usafirisha wa madawa ya kulevya katika mipaka yote ya nchi,vilevile Serikali ifikirie juu kuanzisha mahakama maalum zitakazo shughulikia kesi za madawa ya kulevya.Pia alipendeza bunge kuwa msimamizi wa utekelezwaji wa hukumu kwa kesi za madawa ya kulevya na adhabu iwe imetekelezwa angalau ndani ya wiki mbili. 
Katika maoni kutoka kwa wabunge mbalimbali walisema wanaiomba Serikali kuwa Muswada huu uangalie ni namna gani utalinda haki ya mtu kutoa siri ya mtu atakayetoa taarifa za wafanyabiashara wa Madawa ya Kulevya nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...