Thursday, March 05, 2015

KIJIJI CHA GONGONI WILAYANI KILOSA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WANAWAKE WAPATA HATI MILIKI ZA ARDHI

Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty Alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi, Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
 Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongea na wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ikiwa ni wiki ya maadhimisho hayo, alipongeza harakati za kuwawezesha wanawake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umiliki wa Ardhi, ambapo alisema kuwa OXFAM itahakikisha kila aliyeomba hati ya Kumiliki Ardhi ataipata, pia ameshukuru Taasisi zengine zisizo za kiserikali kuendelea kusaidiana ili kuleta maendeleo.

 Meza Kuu wakifurahia Burudani 
 Burudani ikiwa inaendelea 
 Baadhi ya wanakijiji wakipokea Hati Miliki za Ardhi
Wanakijiji wakipata vijarida
 Wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo
Hata watoto walikuwa bize wakisoma Vipeperushi na Vijarida

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...