Saturday, March 07, 2015

KINANA AKUTANA NA WANACCM KUTOKA SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU MJINI DODOMA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakati alipowasili katika jengo la CCM la White House mjini Dodoma akianza ziara katika Dodoma mjini ambapo amekuwa na kikao na wanafunzi wanachama wa CCM kutoka  Shirikisho la Vyuo vikuu Katikati ni Katibu Mtendaji wa shirikisho hilo Bw. Christopher Ngubiagai na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA)2Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi naMkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakifurahia jambo wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiongoza mkutano wa Wanachama wanafunzi wa CCM Kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu uliofanyika kwenye ukumbi wa White Huouse mjini Dodoma, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa, Lwitiko Stephen Mwenyekiti wa Shirikisho  na kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la vyuo vikuu Bw. Christopher Ngubiagai.4Baadhi ya wanafunzi wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM hayupo pichani wakati alipowasili katika ukumbi wa mkutano.57
13
Viongozi wa kikundi cha vijana wasomi cha New Generation Network cha mjini Dodoma  wakionyesha cheki ya shilingi milioni 10 waliyokabidhiwa na afisa vijana mkoa wa Dodoma Tumsifu Mwasamale  kutoka mfuko wa vijana  wa  Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Maendeleo ya vijana.  Huku Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakipiga makofi.
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na mwenyekiti wa Shirikisho la  Vyuo Vikuu Bw. Lwitiko Stephen.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...