Friday, March 06, 2015

KAMATI YA BUNGE HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA (LAAC) YANYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU

Mweka Hazina wa halamashauri ya wilaya ya Mbulu Nicolaus Harabu  akijibu hoja mbele ya kamati ya hesabu za serikali ya mitaa LAAC ilipotembelea kukagua miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge Hesabu za serikali za Mitaa(LAAC) Azza Hamad akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakati kamati hiyo ilipotembelea halmashauri kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Michael Hadu akijibu hoja mbele ya kamati hiyo.
Mjumbe wa kamati ya LAAC na Mbunge wa viti maalumu vijana,Tauhida Nyimbo akihoji jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilipokutana na watendaji wa Halamashauri ya wilaya ya Mbulu. 
Mjumbe wa kamati ya LAAC na Mbunge wa jimbo la Karatu Mch,Izrael Natse akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mbunge wa jimbo la Mbulu ,Mustapher Akonay akichangia jambo katika kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa (LAAC) wakiwa katika eneo ilipojengwa shule ya sekondari Singland kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba ya mwalimu.
Moja ya jengo ambalo ujenzi wake unaendelea katika shule ya sekondari Singland.
Baadhi ya vyumba vya madarasa ambavyo ujenzi wake unadaiwa kujengwa chini ya kiwango.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu akimuongoza Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa (LAAC) Azza Hamad kukagua majengo katika shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu ,Mustapher Akonay akionesha sehemu ya wazi katika mlango uliofiungwa katika moja ya darasa katika shule hiyo ,mlango unaodaiwa kutengezwa kwa thamani ya shilingi 700,000.
Huu ndio mlango wa sh Laki saba.
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya LAAC ,Azza Hamad akihoji vioo vilivyowekwa katika jengo la darasa moja wapo kama ukubwa wake unaendana na ule ulioko kwenye kitabu cha makadirio ya thamani ya mradi.
Mhandisi wa Ujenzi wa Halamashauri ya Mbulu ,Elias Bilomo akijaribu kutizama katika kitabu chake ukubwa wa vioo ulioelekezwa kuwekwa katika jengo hilo kama unaendana na ule uliopo.
Kamati ikiendelea na ukaguzi katika mradi wa maji wa kijiji cha Masieda.
Mjumbe wa kamati ya LAAC na mbunge wa jimbo la Mbogwe ,Agustino Masele akijaribu kufungua maji katika mradi wa Masieda
Mjumbe wa kamati ya LAAC na Mbunge wa Mufindi ,Menrad Kigola akiuliza jambo wakatika kamati hiyo ilipotembelea mradi wa maji wa Masieda.
Kamati ya Bunge Hesabu za serikali za Mitaa ikatembea zahanati ya Daudi.
Wajumbe wakiangalia vitanda katika moja ya wodi katika zahanati hiyo.
Chumba cha daktari katika zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ,Azza Hamadi akitoa maagizo kwa Halamashauri ya wilaya Mbulu katika kikao cha majumuisho.
Baadhi ya Wajumbe na watumishi wa Halamashauri ya wilaya ya Mbulu.
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Manyara Mwajabu Nyamkola akitoa neo la shukrani mara baada ya kukamilika kwa kikao  cha kamati ya LAAC.
Mbunge wa jimbo la Mbulu ,Mustapher Akonay akizungumza jambo katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...