Tuesday, February 03, 2015

WASANII KUTOKA TANZANIA WATUMBWIZA MASCUT-OMAN

1
Hussen Ferej akiwajibika jukwaani wakati Watanzania walipokuwa wanatumbwiza Ngoma aina ya “Kitua tua” katika Jukwaa kuu la Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
5
Wasanii wa Ngoma ya Msewe kutoka Tanzania wakitumbuiza katika Jukwaa kuu kwenye Maonesho yanayoendelea ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni,Muscut –Oman.Wasanii hao watakuwa wakitoa burudani hiyo kwa wiki mbili
1011
Baadhi ya Mashabiki wakitazama burudani iliyokuwa ikitolewa na Wasanii kutoka nchi tofauti duniani zinazoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni, nchini Oman,
…………………………………………………………………………………..
Na Faki Mjaka, Mascut Oman
Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut nchini Oman yamechukua sura mpya baada ya Nchi Washiriki kupeleka Wasanii wake wa Ngoma za Asili kwenda kutumbwiza katika wiki mbili za mwisho ya Maonesho hayo.
Tanzania ni moja ya nchi washiriki ambapo Wasanii wake 15 Usiku wa jana walipata nafasi ya kuburudisha kwenye Jukwaa kuu la Maonesho hayo.
Akizungumza kuhusu ujio wao Kiongozi wa Wasanii hao wa Ngoma Bi Asha Khatib amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanazikonga vyema nyoyo za Waomani kwa burudani ya nguvu.
Amefafanua kuwa Waoman wengi wanapenda Ngoma zenye asili ya Zanzibar hivyo wamefanya Mazoezi ya kutosha ili kuwafurahisha Mashabiki wao pale wanapopanda Jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza.
“Kwa kweli tumejiandaa vizuri tu na tumekuja hapa Mascut kwa kazi moja tu ya kutoa Burudani hivyo Waoman wazidi kuja kwa wingi kuja kujionea burudani ya aina yake yenye Asili ya Tanzania-Zanzibar”Alisema Bi Asha.
Bi Asha amebainisha kuwa katika Jukwaa watapiga baadhi ya Ngoma zenye Asili ya Zanzibar kama vile Msewe, Uringe, Gonga, Kyaso,Kitua tua,Kibunguu na Kidumbaki ambapo anaamini zitakidhi kiu ya burudani kwa Waomani.
Jana ikiwa ni siku ya mwanzo kwa Watanzania hao hivyo walipewa muda wa nusu saa kwa ajili ya kusalimia jukwaa na kutumbuiza ambapo walipiga Ngoma ya Msewe na Kitua tua.
Kabla ya Watanzania kupanda Jukwaani kwenda kutumbuiza walitanguliwa na Wasanii kutoka Ufaransa ambapo baada ya Watanzania kumaliza Wasanii kutoka Urusi ndio waliochukua nafasi kutumbuiza.
Nchi nyingine zilizopata nafasi ya kutumbuiza katika Jukwaa kwenye Maonesho hayo ya Kimatifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni ni pamoja na China, Iran, Thailand, India, Uzbekistani na Misri.
Kwa wiki mbili mfululizo kuanzia jana Wasanii wa Nchi hizo zinazoshoriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni watakuwa wakipanda katika Jukwaa kuonesha vipaji vyao vya Muziki wa Asili ya nchi zao husika.
Wasanii hao wa Ngoma waliofika Juzi kutoka Tanzania wanaungana na Wenzao waliokuwepo Oman kwa zaidi ya wiki mbili sasa kushiriki Maonesho hayo ambapo Wasanii huonesha bidhaa zao wanazozitengeneza kwa Mikono na kuwauzia Wateja mbalimbali wanaofika katika Maonesho hayo.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...