Tuesday, February 03, 2015

RAIA WATATU WA KUTOKA NORWAY WAMEJIKUTA MIKONONI MWA BODI YA FILAMU WAKITENGENEZA FILAMU ZA BILA KIBALI

 2
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo( wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu filamu hiyo iliyokuwa ikirekodiwa na raia wa Norway katika Ofisi ya Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam
.3
Raia wa Norway  waliokamatwa wakiwa katika kikao kuhusu filamu waliyokuwa wakirekodi kwenye Ofisi ya Bodi ya Filamu.4
Torshin Nodland raia wa Norway  (watatu kulia) akijitetea kuhusu filamu hiyo waliyokuwa wakirekodi.
1
Baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia raia hao wa Norway katika kurekodi filamu hiyo vikiwa katika Ofisi ya Bodi ya Filamu.
………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Raia watatu wa Norway wamejikuta mikononi mwa Bodi ya Filamu nchini baada kuchukua picha kwa ajili ya kutengeneza makala ya filamu inayohusu kazi za kutafsiri filamu za nje zinazofanywa na Bwana Derick Mukandala maarufu kama Mzee Lufufu maeneo ya Vingunguti.
Wageni hao hawakuwa na kibali cha kutengeneza filamu kinachotolewa na Bodi hiyo hii ni kutokana na kunywimwa kibali kwa makubaliono ya kubadili mswada wa filamu hiyo.Uongozi wa Bodi ya Filamu iliwabaini zoezi hilo katika operesheni zake za kawaida zilizofanyika mwishoni mwa wiki,. 
Miongoni mwa wageni hao waliobainika ni mwandishi wa Mwongozo/Mswada (Script) Bw.Bjorn_Eric Hansen, Mpiga Picha(Cameraman) Bw.Torshin Nodland na mnasa sauti,kutoka Kampuni ya Grunder Film ya nchini Norway.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo alisema filamu hiyo iliyokuwa ikitengenezwa na wageni hao kwa kushirikiana na Kampuni ya Get Real Training ya hapa nchini ilikuwa inahusu kazi anazozifanya Mzee Lufufu zinazokinzana na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya 1976 na pia Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 ya nchi.
Bibi Fisoo aliendelea kusema bodi ya Filamu haiwezi kuruhusu utengenezaji wa filamu hiyo inayoonyesha ukiukwaji wa Sheria kwani kuna kinzana na juhudi za serikali katika kupambana na uharamia wa kazi za filamu na kwamba kamati tayari ilikwisha waandikia wahusika barua ya kuzuia uandaajwi wa filamu hiyo.
“Wajumbe wa kamati ya vibali walielekeza wahusika kubadili maudhui ya mswada wao wakati walipopitia maombi ya kibali jambo ambalo halikukamilishwa. Hii ni kwa sababu mswada wa kutengeneza filamu hiyo unaonyesha kwamba mhusika watakayemtumia ni mtu ambaye amekuwa akikiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999,pamoja na mikataba ya Kimataifa inayosimamia Hakimiliki na Hakishiriki kama vile Mkataba wa Berne ambao Tanzania imeridhia ”,alisema Bibi Fissoo.
Kwa upande wa raia hao wa Norway walikiri kuvunja Sheria na kukiuka taratibu za uandaaji wa filamu katika nchi na kuomba kwenda kubadili mswada wa filamu hiyo kwa mara nyingine ili waweze kuwasilisha upya pamoja na kufuata taratibu za kuomba kibali cha kutengeneza filamu kwa mujibu wa Sheria za nchi na ithibati ya Hakimiliki kutoka COSOTA.
“Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976, iwapo Bodi itadhihirisha ukiukwaji wa sheria hiyo itaamuru tozo la faini papo kwa papo isiyopungua shillingi milioni moja, kuamuru kusitisha utengenezaji wa picha jongevu husika au kuamuru mkosaji kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria”alisema Bibi Fissoo.
Kwa niaba ya wenzake Bw.Hansen alisema wameipokea faini hiyo na wanaahidi kulipa faini mara moja na kuwasilisha risiti, aidha walioomba radhi kwa kosa hilo na kuahidi kutotumia picha hizo mahali yoyote.
Katika kuthibitisha raia hao wa Norway hawataendelea na zoezi la uchukuaji wa filamu hiyo, Bodi ya Filamu iliwekaana makubaliano nao kwa maandishi kuwa kutoendelea kupiga picha hizo hadi pale watakapobadilishi muswada wao na kupewa kibali cha kutengeneza filamu.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...