Kutoka kushoto wengine ni Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA)Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Songea mjini Bw. Joseph Mkirikiti wakati alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kushoto ni Mh. Said Mwambungu Mkuu wa mkoa wa Ruvuma.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akitaniana na Mbunge wa jimbo la nyasa Mh. Kapteni John Komba.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wakuuu wa vyombo vya ulinzi na usaliama wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege Songea mkoani RuvumaMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma mbalimbali zilizokuwa zikitumbuizwa na vikundi mbalimbali vilivyompokea leo kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Ruvuma kulia ni John Komba mbunge wa jimbo la Nyasa na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida ndugu Mgana Msindai na Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Ndugu Joseph Mkirikiti.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh Mwigulu Nchemba akipokelewa na Nape nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Majimaji.
Star Tv wanastahili kupongezwa kwa kazi waliyoifanya leo kwani kazi yao ilikuwa imetulia na imepongezwa na watu wengi waliokuwa wakifuatilia kwenye luninga huyu ni mmoja wa wapigapicha wa kituo hicho akifanya vitu vyake. Baadhi ya wazee waliofika kwenye maadhimisho hayo wakipelekwa eneo la kukaa.Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM bara katikati, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Dr. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakimsubiri Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya Kikwete kuwasili.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa Majimaji huku akiwapungia mikono wana CCM na wananchi aliojitokeza katika maadhimisho hayo yaliyofana.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa majimaji.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akivishwa skafu na vijana wa chipikizi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kwa kuimbiwa wimbo wa taifa na vijana wa chipukizi.baadhi ya vijana wa chipukizi wakiimba wimbo wa taifa kwenye uwanja wa Majimaji katika maadhimisho hayo yaliyofana.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana kulia pamoja na wanakamati ya maandalizi wakiimba wimbo wa taifa.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la chipukizi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea tayari kwa kuongoza maadhimisho ya miaka 38 ya CCM mkoani Ruvuma Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la chipukizi.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dr. Jakaya Kikwete akipokea heshima wakati gwaride la heshima la Chipukizi likipita na kutoa heshimza zake kwenye jukwaa kuu.Gwaride la heshima likipita mbele ya jukwaa kuuu na kutoa heshima.Mpiganaji wa kituo cha Televisheni cha Star TV akifanya vitu vyake katika katika maadhimisho hayo. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NDugu Nape Nnauye akizungumza jambo katika maadhimisho hayoUmati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho hayo.Kapteni John Komba kulia na Abdul Misambano wa TOT wakiimba katika maadhimisho hayo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Songea mkoani Ruvuma wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya CCM.Mwanamuziki Diamond Plutnamz akiimba katika uwanja wa Majimaji wakati wa maadhimisho ya miaka38 ya CCM mjini Songea mkoani Ruvuma.Mwanamuziki Diamond Plutnamz akcheza katika uwanja wa Majimaji wakati wa maadhimisho ya miaka38 ya CCM mjini Songea mkoani Ruvuma.Mkuu wa wilaya ya Songea mjini Mh. Joseph Mkirikiti akiwapooza wananchi wa Songea kutulia ili Diamond Plutnamz kufanya vitu vyake jukwaani.
No comments:
Post a Comment