Monday, September 08, 2014

SERIKALI YA WATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA MAWASILIANO.

…………………………………………………………………
Serikali yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi mabaya ya Mawasiliano na udanganyifu katika usajili wa namba za simu za mkononi kwa kuwa ni kosa la jinai.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) bw. Innocent Mungy amesema kumekuwa na watu wachache wanaotumia mawasiliano pasipo kuzingatia sheria na kanuni.Kumekuwa na matukio yanayoashiria kutumika kwa mitandao ya kijamii kuleta madharambalimbali kwa watumiaji ikiwemo utapeli,kulipiza kisasi, ugomvi,kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli na kuvuruga kwa ujumla alisema MungyAkifafanua Mungy amesema pamoja na maendeleo chanya katika Sekta ya Mawasiliano kumekuwa na watu wachache wanaotumia simu,mitandao ya kijamii,redio,televisheni,  na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani.
Kutokana na hali hiyo Mungy amesema kuwa TCRA inawakumbusha wananchi wote kwamba ni kosa la jinai kutumia mawasilano vibaya kama ilivyoainishwa kwenye  sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta ( EPOCA) ya mwaka 2012.
Pia Mungy alitoa wito kwa wananchi na watumiaji wa simu za mkononi kuunga mkono juhudi za Serikali ili wananchi wote wasajili namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani ,usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta hii na Taifa kwa ujumla.Naye Naibu Mkurugenzi Masuala ya Huduma kwa wateja toka mamlaka hiyo Bw. Isaac Mruma amesema ni vyema wananchi wakazingatia matumizi sahihi ya mawasiliano kwa maslahi mapana na Taifa.Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) mwaka 2010, kifungu cha 131 imeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika kwa namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano (Tsh. 500,000) au kifungo cha miezi mitatu kwa atakayekiuka sheria hii

No comments:

Rais Samia Aongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma

Dodoma, 18 Januari 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameo...