Serikali yatoa usajili kwa makampuni 51 ya wakala Binafsi wa Huduma za ajira nchini kati ya 87 yaliyowasilisha maombi yake kwa Kamishna wa kazi.Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwan Wema wakati wa mkutano na waansishi wa habari.
Makampuni yaliyosalia 36 hayakupata usajili kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokidhi vigezo na kukosa nyaraka muhimu. Alisema wema.Akitaja baadhi ya makampuni yaliyopewa usajili baada ya kukidhi vigezo kuwa ni PA Ppospect Africa,Delloitte,KPMG Advisory Ltd, People Ltd, HR-Solutions na AGP Consultants.
Akifafanua wema amesema kuwa Kampuni au wakala yoyote ambaye hajapata usajili hatoruhusiwa kufanya kazi ya uwakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini.Katika Kushughulikia suala la usajili Wema amesema kuwa Wizara imeandaa kanuni chini ya sheria ya ukuzaji wa huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na kutangazwa kupitia tangazo la Serikali Na. 232 la tarehe 11 Julai 2014.
Aidha Wema alitoa wito Makampuni au mtu yeyote anayetaka kufanya shughuli za huduma za ajira kuzingatia taratibu na kanuni chini ya Sheria ya kukuza Huduma za ajira Na. 9 ya Mwaka 1999.
Katika hatua nyingine Wema amesema kwamba ukodishaji wa Huduma (outsourcing of Services) haujapigwa marufuku bali kilichopigwa marufuku ni ukodishwaji wa watu (outsourcing of persons) hivyo ni marufuku kwa wakala wa huduma za ajira kuajira na kukodisha wafanyakazi au kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine na wakala hao kuwa sehemu ya mahusiano ya ajira yanayoweza kujitokeza baina ya watafuta kazi na waajiri.
No comments:
Post a Comment