Habari za hivi punde kutoka Mkoani Morogoro zinapasha kuwa basi la Kampuni ya Airbus lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Tabora limepata ajali muda si mrefu eneo la Kiegeya Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.
Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile ameiambia Father Kidevu Blog kuwa ni kweli kuna ajali nae yupo eneo la tukio.
“Ninaomba unitafute baade kidogo kwa taarifa kamili kwa sasa nipo eneo la ajali huku Gairo,” alisema SACP Shilogile.
tunafuatilia zaidi kuhusiana na tukio hilo ambalo linaelezwa kugharimu uhai wa watu zaidi 10
No comments:
Post a Comment