Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia
Mchechu na ujumbe wake wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bw. Abdulah Lutavi
akiwatembeza kwenye eneo lililotengwa na Wilaya hiyo kwa ajili ya kujengewa
nyumba na NHC. Shirika la Nyumba litajenga nyumba za gharama nafuu katika
halmashauri hiyo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu, Mkuu wa Wilaya Natumbo, Bw. Abdulah Lutavi na ujumbe wao wakijadiliana kwenye eneo litakalojengwa nyumba za gharama nafuu na Shirika la Nyumba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu na msafara wake wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wa Mkuzo, Songea. Mradi huo una jumla ya nyumba 18.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu akizugumza na Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kuhusu mpango wa NHC wa kuwekeza ujenzi wa nyumba katika halmashauri hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu akiongea na Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma na Shirika la Nyumba la Taifa na kulihakikishia Shirika kupewa viwanja vya kujenga nyumba katika halmashauri zote za mkoa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu akisikiliza maelezo ya kiongozi wa kikundi cha vijana Peramiho.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu akishiriki katika ufyatuaji wa matofali na vikundi vya vijana wilayani Peramiho mwishoni mwa wiki.
Ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu ukitembezwa katika maeneo
yenye viwanja katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia
Mchechu na ujumbe wake wakionyeshwa viwanja na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbinga, Bw. Julius Mwakafwila vitakavyotumika kujenga nyumba za
gharama nafuu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na Watendaji wa wilaya ya Mbinga na NHC wakati akiagana na ujumbe wa Halmashauri ya Mbinga mwishoni mwa wiki
No comments:
Post a Comment