TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, Septemba 8, 2014
BIA ya Kibo Gold Lager imechaguliwa kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwa ubora duniani inayotolewa na ‘Monde Selection’. Kibo ilipokea utambulisho huo wa kimataifa wakati wa sherehe za 53 za kila mwaka zilizofanyika huko Bordeaux, Ufaransa.
‘Monde Selection’ ni tuzo zinazotolewa kila mwaka tangu mwaka 1961, kwa ajili ya bidhaa za vinywaji na chakula. Huendeshwa na kampuni ya Biashara ijulikanayo kama ‘International Institute for Quality Selections’ ya Brussels, Ubelgiji. Bidhaa hizo huonjwa na kujaribiwa ili ziweze kupewa alama ya ubora.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL), Bw. Steve Ganon, alisema: “Kama familia ya SBL, tumefarijika sana kusikia habari hii kubwa inayoihusu bidhaa yetu, kitu kama hiki huwa hakitokei hivi hivi; tumekifanya kitokee… Kwa hiyo ninaipongeza timu nzima ya SBL kwa juhudi zao za kujenga imani kwa watumiaji.”
Bia ya Kibo Gold ilizinduliwa miaka 15 iliyopita chini ya Kibo Breweries. Kwa bahati mbaya, bidhaa hiyo haikudumu sana sokoni kutokana na kufungwa kwa kampuni ya Kibo Breweries. Nembo hiyo ilichukuliwa na Serengeti Breweries Ltd na kuzinduliwa upya Juni 2012 katika kiwanda cha SBL kilichopo Moshi Brewery ambako ndiko huzalishwa na kusambazwa sehemukubwa ya kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kati ya mingine mingi.
Lengo la bia ya Kibo Gold ni kutanua wigo wa vinywaji vya Serengeti Breweries Ltd na kuwashika watumiaji wa daraja la kati katika soko la kaskazini mwa nchi.
Agosti 2013, Kibo Gold ilibadilishwa na kuwekwa katika chupa yenye shingo ndefu maarufu kama ‘mwanamke nyonga’ ili kwenda na wakati na matakwa ya soko la kisasa.
Sasa Kibo ipo katika chupa yenye shingo ndefu ya milimita 500 ikiwa na asilima 5.5 ya kileo inayodumu kwa kipindi cha miezi sita. Kauli mbiu ya Kibo ni ‘Yaone maisha katika mwanga bora.’
Bia hii kwa sasa inauzwa rejareja kwa Sh 1,800
No comments:
Post a Comment