Tuesday, September 09, 2014

JOPO LA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI LAFANYA ZIARA KATIKA MGODI WA GEITA GOLD MINE

Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine uliopo mkoani Geita. Mgodi huu ni moja ya makampuni yanayowania tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya serikali na jamii Bw. Clement Msalangi (mbele kwa mbali) akielezea mafanikio ya mgodi wa Geita Gold Mine katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na uwezeshaji kwa timu ya majaji na sektretarieti iliyofanya ziara katika mgodi huo.
Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma akisisitiza jambo katika kikao kilichoshirikisha uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyotembelea mgodi huo.
Mtaalamu katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima ( wa pili kutoka kulia) akielezea mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika mradi wa maji mbele ya bwawa la Nyankanga ambalo maji yake yatasafishwa na kusambazwa kwa wananchi wa Geita kupitia ufadhili wa mgodi huo.
Mtaalamu katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima ( wa kwanza kulia) akitoa maelezo juu ya mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa kisima mbele ya timu ya majaji na sekretarieti iliyotembelea mradi huo.
Afisa Afya Mkuu wa mgodi wa Geita Gold Mine Dkt. Kiva Mvungi ( wa pili kutoka kulia) akielezea mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa kituo cha upimaji wa virusi vya Ukimwi na utoaji wa ushauri nasaha cha Geita mbele ya baadhi ya majaji na watendaji wa mgodi huo waliotembelea kituo hicho.
Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma (katikati) akielezea majaji na sekretarieti mchango wa mgodi wa Geita Gold Mine katika ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya wakazi wa Geita waliohamishwa kwa ajili ya kupisha shughuli za mgodi huo.
Mtaalamu katika masuala ya mahusiano na maendeleo ya jamii Bw. Joseph Mangilima ( wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele) akiongoza timu ya majaji, sekretarieti na wataalamu wengine kutoka mgodi huo katika ziara kwenye kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma, kinachofadhiliwa na mgodi huo.

No comments:

Rais Samia Aongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma

Dodoma, 18 Januari 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameo...