Na Jeff Msangi
wa TBN Ughaibuni
Nyota njema huonekana asubuhi. Bila shaka umewahi kusikia msemo huu. Kwa Zahara Muhidini Issa Michuzi, nyota yake njema ni tunu ya uongozi. Tangu alipoweza kutambua maana na tofauti ya jambo jema na baya, amekuwa kiongozi.
Muhtasari wa maisha yake unaonyesha alizaliwa mnano tarehe 2 Septemba mwaka 1987 Nzega mkoani Tabora. Amesomea katika shule zifuatazo;
*Shule Ya Msingi Rufita, Tabora- 1995-2001
*Shule Ya Sekondari Kazima, Tabora-2002-2005
*Shule Ya Sekondari Ya Juu Emma, Kampala-Uganda 2007-2009
*Chuo Kikuu Cha Dodoma, Dodoma,Tanzania 2011-2014.
Zahara Muhidini Issa Michuzi, ambaye ni binti wa Ankal, ni mhitimu wa Shahada ya Sanaa katika masuala ya Uchumi. Mpaka kufikia hapa alipo, nyota yake ya uongozi imejidhihirisha katika sehemu mbalimbali alizopitia hususani shule.
Amekuwa kiranja, msimamizi wa shughuli na miradi mbalimbali shuleni na alipokuwa Chuo Kikuu Dodoma alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Wanafunzi- University of Dodoma Students Organization (UDOSO) akiwa kama Mbunge wa Baraza La Wanafunzi.
Mbali ya uzoefu wa kiuongozi alionao, Zahara anazo sifa zifuatazo ambazo ni nadra na tunu kubwa katika uongozi;
Anajitambua– Zahara anajitambua vilivyo. Anatambua kwamba uongozi ni heshima na utumishi uliotukuka.
Ana Ari Ya Kuongoza na
Kujifunza– Zahara anaamini kwamba kiongozi bora lazima awe ana ari ya kuongoza na kutumikia wananchi anaowaongoza. Mbali ya kuongoza,kiongozi lazima awe tayari kujifunza kutokana na hali halisi na kukabiliana na mabadiliko ya aina yoyote yanayoweza kujitokeza.
Ni Msikivu Na Ana uwezo Mkubwa wa Kufanya Kazi na Watu– Hili Zahara amelithibitisha katika ngazi zote za kiuongozi ambazo amepitia. Usikivu wake umekuwa chachu ya kumwezesha kutatua matatizo mbalimbali ambayo amekabiliana nayo huku yeye kama kiongozi akitarajiwa kuyatatua.
Ana Uwezo Wa Kuongoza Mabadiliko Ya Kijamii– Zahara anaamini kwa vitendo kwamba jamii yoyote lazima isonge mbele ili kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali ya kijamii. Anaamini kwa vitendo kwamba uongozi thabiti unahitajika ili kuleta mabadiliko chanya ambayo jamii yoyote inahitaji.
Zahara Muhidini Issa Michuzi hivi sasa anagombea kuwa mwakilishi wa vijana Bungeni kupitia Viti Maalumu Vijana (Youth Seats) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)- Tabora. Anaomba Kura na Ushirikiano Wako.
Ankal akifurahi na binti yake Zahara siku ya Maulid maalumu ya kusherehekea kuhitimu digrii ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka jana. Hii ndiyo siku ambayo Zahara aliweka nia hadharani kwamba angependa kugombea Ubunge mkoani Tabora ili kumuenzi marehemu mama yake kwa kuwatumikia wananchi wa mkoa huo kwa moyo wake wote.
Zahara akifurahi na Mama yake mlezi |
No comments:
Post a Comment