Wednesday, February 04, 2015

WIZARA YA MAJI KUPITIA BRN IMEFIKISHA MAJI KWA WANANCHI M.4.2

IMG-20150203-WA0039
Waziri wa maji profesa jumanne maghembe akielezea utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini.
…………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Waziri wa maji kupitia mpango wa BRN,kuanzia mwaka 2013 hadi sasa,imefanikiwa kuwafikishia maji wananchi milioni 4.3 wanaoishi maeneo ya mijini
Aidha zaidi ya watu milioni 2 wanaoishi maeneo ya vijijini wamepatiwa huduma ya maji kupitia BRN
Waziri wa maji profesa jumanne maghembe ameyasema hayo Februari 3, 2015  mjini Dodoma alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini ya wizara ya maji katika ukumbi wa Fr.Vicent uliyopo ndani ya hotel ya St.Gasper
Profesa Maghembe amesema kuwa,mpango huo wa BRN umeonyesha kwa muda mfupi tofauti na ule mpango wa Taifa wa maji uliyonza mwaka 2017 hadi mwaka 2014
Amesema serikali kupitia mpango wa BRN itahakikisha inawafikishia wananchi maji katika maeneo mbali mbali ili kuwapunguzia kero ya maji
Kadhalika Maghembe amewataka wafanyakazi wa mamlaka za maji hapa nchini kufanya kazi kwa kasi kubwa na sio mazowea
Katika mkutano huo viongozi wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira za miji mikuu ya mikoa zimetia saini makubaliano ya miradi ya maji na mazingira kwa kutumia utaratibu wa BRN

No comments:

WASSIRA ATEMBELEA KABURI LA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE BUTIAMA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira ametembelea kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage ...