Tuesday, February 03, 2015

TASWIRA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira James Lembeli akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Kamati yake kwa Kipindi cha Mwaka 2014, Bungeni mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Said Nkumba akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akijibu maswali wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni leo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela akijibu maswali ya wabunge.
Baadhi ya Mawaziri wakiwa kwenye ukumbi wa Bunge.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Juma Nkamia Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Diana Chilolo akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Mahakama ya Wilaya ya Iramba mkoni Singida.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola akichangia taarifa za kamati zilizowasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma
Baadhi ya wageni ambao ni wanafunzi wa Shule ya Awali ya Mchepuo wa Kiingereza ya Labi ya mkoni Dodoma wakiwa na walezi wao, wakifuatilia Bunge. Picha na Lorietha Laurence-MAELEZO, Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira (kulia) akijadili jambo na wabunge wenzake baada ya kuahirishwa kikao cha asubuhi Bungeni mjini Dodoma.Wengine kutoka kulia ni Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid akijadili jambo na Mbunge wa viti maalum Margaret Sitta, nje ya ukumbi wa Bunge.
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akizungumza na Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji baada ya Bunge kuahirishwa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...